BABU HUYU ALIKUWA BALAA KWA MIDADI WAKATI AKIKUNG'UTA NGOMA
MAMA HUYU ANASEMA SASA BASI KWENDA KWA WAKUNGA WA JADI , DALILI ZINAZOONYESHA KUWA WANA MATUMAINI MAKUBWA NA HUDUMA ZA AFYA KIJIJINI MWAO
HII NDIYO BENDI YA ZAKALE NI DHAHABU AMBAYO ILIKUWA IKITOA BURUDANI KWENYE MAADHIMISHO HAYO HUKU KIKOSI KIKIUNDWA NA WATU WENYE UMRI WA KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA!
MZEE HUYU NAYE ALIKUWA MWANAKWAYA JANA
AKINA MAMA WAKITOA USHUHUDA WA MATUKIO YA VIFO NA CHANGAMOTO WALIZOPITIA KABLA YA KUKOSA HUDUMA ZA MATIBABU KIJIJINI KWAO
MGANGA MKUU WILAYA YA MBOZI DR CHARLES MKOMBACHEPA AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI HUO, KUSHOTO KWAKE NI KATIBU WA AFYA WILAYANI MBOZI MZEE MROSSO NA KULIA KWAKE NI KATIBU TAWALA WILAYA BWANA LAZARO MWANKENJA
JENGO LA ZAHANATI ILIYOZINDULIWA JANA KATIKA KIJIJI CHA MSAMBA I WILAYANI MBOZI
Na Danny Tweve -Mbozi
ASILIMIA 65 YA WANAWAKE
WAJAWAZITO WILAYANI MBOZI MKOANI MBEYA BADO WANAJIHUJIFUNGULIA MAJUMBANI NA KWA
WAKUNGA WA ASILI HALI AMBAYO
INASABABISHA KUCHANGIA VIFO VINGI VYA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA KUTOKANA NA KUKOSEKANA KWA HUDUMA RAFIKI NA ZA
KARIBU ZA UZAZI SALAMA.
TAKWIMU ZA WILAYA ZINAONYESHA NI ASILIMIA 42 HADI 47 TU YA WANAWAKE WANAOJIFUNGULIA KATIKA VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI HUKU KUNDI KUBWA LIKIJISALIMISHA KWA WAKUNGA WA JADI NA WAGANGA WA KIENYEJI
HALI HII IMEELEZWA KUCHANGIWA NA UKOSEFU WA ELIMU NA HUDUMA HIZO KUWA MBALI NA WANANCHI
HAYO YAMEBAINISHWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA MSAMBA I
WILAYANI MBOZI AMBAPO WAMEREJEREA BAADHI YA MATUKIO YA HIVI KARIBUNI YA VIFO
VYA WAJAWAZITO NA KWAMBA DHANA YA KILA KIJIJI KUWA NA ZAHANATI HAIPASWI KUPUUZWA
KWA SASA KUTOKANA NA UKWELI KWAMBA CHANGAMOTO ZA MASUALA YA UZAZI
NA MAGONJWA YA WATOTO VIJIJINI NI
NYINGI KUTOKANA NA KUKOSEKANA ELIMU YA AFYA YA MSINGI NA UZAZI SALAMA .
AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUFUNGUA ZAHANATI ILIYOJENGWA KWA NGUVU ZA WANANCHI KIJIJINI
HAPO MGANGA MKUU WA WILAYA YA MBOZI DR CHARLES MKOMBACHEPA AMESEMA, TAKWIMU ZA
VIFO VYA WATOTO NA WAJAWAZITO PAMOJA NA
KIWANGO CHA HUDUMA ZA CHANJO ZINAONYESHA KUWEPO PENGO KUBWA LA HUDUMA KWA
MAKUNDI HAYO ..
NAYE KATIBU TAWALA WA WILAYA MBOZI LAZARO MWANKENJA AMBAYE
ALIMWAKILISHA MKUU WA WILAYA MBOZI KWENYE UFUNGUZI HUO AMEWATAKA WANANCHI
KUJIELEKEZA KATIKA KUJENGA MIUNDO MBINU YA HUDUMA MBALIMBALI KWA NJIA YA
KUJITOLEA ILI KURAHISISHIA SERIKALI KUELEKEZA RASLIMALI KATIKA UMALIZIAJI NA
VITENDEA KAZI..
ZAHANATI HIYO KULINGANA
NA RISALA ILIYOSOMWA NA BWANA
JONATHAN MWAISWELO INALENGA KUTOA HUDUMA KWA WAKAZI 2,500 WA KIJIJI HICHO HUKU PIA IKIWA NI FULSA MUHIMU KWA VIJIJI JIRANI VYENYE WAKAZI ZAIDI YA 6500
MUDA WOTE AKINA MAMA WALIKUWA WAKIIMBA NYIMBO NA KUFURAHIA HII IKIONYESHA KUCHOSHWA NA CHANGAMOTO ZA VIFO NA MAGONJWA MBALIMBALI KULIKOCHANGIWA NA KUKOSEKANA KWA HUDUMA ZA MATIBABU KWA KARIBU.
MWISHO