Adverts

Feb 15, 2013

MWAKYEMBE AVAMIA TUNDUMA GHAFLA Mwakyembe akisisitiza jambo wakati akizungumza na madereva  kando ni mkuu wa wilaya ya Momba ABIUD SAIDEA
 Pilika za boda

 MADEREVA WAKISHANGILIA BAAA YA KUAMBIWA MPAKA UTAFANYA KAZI SAA 24
 GHAFLA PROFESA MAJI MAREFU  MBUNGE WA KOROGWE AKATOKEA! HAPA AKITAMBULISHWA NA MWAKYEMBE AKIMBATANA NA MCHUNGAJI MWANJALI LACKSON MBUNGE WA MBEYA VIJIJINI 
 NAYE MAGRET SITA ALIKUWEPO- MBUNGE VITI MAALUM TABORA
Waziri wa Uchukuzi Mh Mwakyembe jana amevamia mji wa Tunduma kwa lengo la kujionea hali ya msongamano wa magari na kufanya mazungumzo na madereva pamoja  na wamiliki wa maroli yanayofanya safari zake ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika eneo la ofisi za Uhamiaji Tunduma, Mwakyembe amesema hatua zinazochukuliwa hivi sasa ni kuimarisha usafiri wa reli ya TAZARA na kwamba, hatua hiyo itazinusuru barabara na kupunguza msongamano katika mji wa Tunduma
Aliwatoa hofu madereva wa maroli makubwa kwamba hatua hizo hazilengi kuwamaliza kimaisha kwakuwa watakosa ajira na kwamba bado kuna kazi nyingi za usafirishaji ndani ya nchi kwaajili ya kuwezesha mizigo kusogezwa kwenye usafiri wa reli ambapo shughuli za uchukuzi na usafirishaji ni kiungo muhimu cha uchumi mahala popote duniani.

Amesema hatua nyingine iliyochukuliwa ni pamoja na makubaliano ya nchi zote zinazotumia mpaka wa Tunduma yaani Zambia na Tanzania kufanya kazi saa 24 hivyo kuwezesha taratibu za clearance kufanyika kwa wakati

Taarifa hiyo ilishangiliwa na madereva ambao wanaonekana kuchoshwa na mifumo ya huduma za masaa 11 kutokana  na kutofautiana baina ya Zambia na Tanzania katika uhesabuji wa masaa ya kazi kutokana na kuwa katka kanda tofauti(east and central).

Kwa upande wa TANZANIA utoaji huduma eneo la mpakani kwa saa 24 itaanza mwezi June, 2013 wakati Zambia wametangaza kuwa tayari wakati huu.
Aidha kero nyingine aliyoelezwa mh Mwakyembe ni pamoja na ucheleweshaji wakati wa ukaguzi wa mizigo ambao unatokana na matumizi ya mifumo ya zamani (zana hakuna) tofauti na Upande wa Zambia ambao wapo kwenye hatua za mwisho kufunga scanning machine itakayowezesha kukagua kwa dakika chache gari lnapovuka.
Tayari Zambia wamefunga mitambo hiyo katika mipaka yao na Zimbabwe na Msumbiji ambapo kwa upande wa Zimbabwe katika mpaka wa Chilundu mtambo huo ulizinduliwa miaka mitatu iliyopita