Na Danny Tweve wa Indabaafrica blog
Wilaya nne za
Tanzania na Mbili za nchini Malawi zitanufaika na miradi mikubwa inayokusudiwa
kuanzishwa kupitia mto songwe itakayogharimu Euro 400 Milion (zaidi ya Trilion
moja za Kitanzania) katika kipindi cha
miaka kumi kuanzia mwezi march mwaka huu.
Miradi hiyo imeibuliwa ikiwa ni
sehemu ya suluhisho lakudumu la maafa ya kuhama hama kwa mto songwe na
kusababisha upotevu wa mali, uhai wa watu na pia mipaka baina ya Tanzania na
Malawi kuhama hama kila msimu wa mafuriko ya mto huo
Akitambulisha hatua za
utekelezaji wa Program ya Maendeleo ya Bonde la Mto Songwe , mratibu wa program hiyo upande wa Tanzania Mhandisi
Gabriel Kalinga ambaye pia aliongozana na afisa wa upande wa Malawi pamoja na Meneja wa Program hiyo kwa ujumla faida za awali ya miradi hiyo mikubwa
ni pamoja na ujenzi wa mabwawa matatu kwa upande wa Tanzania yatakayozalisha
umeme Megawati 430
Vivyo hivyo kwa upande wa Malawi
wilaya za Chitipa na Kalonga zitanufaika na miradi hiyo ambapo pia jumla ya
mabwawa matatu yatajengwa na kuzalisha umeme pamoja na fulsa nyingine za
kiuchumi ikiwemo kilimo cha umwagiliaji.
Kulingana na matakwa ya mpango
huo miongoni mwa hatua muhimu za utekelezaji wa hatua ya pili ya program huyo
ni pamoja na kubaini wadau wa Bonde husika na hatimaye kutambulisha nia ya
utekelezaji wa mradi huo ili waweze kutoa maoni yao, hatua ambayo ujumbe huo
umeendelea kufanya kwa wilaya za Kyela, Rungwe, Mbozi na Ileje.
Mhandisi Kalinga alisema tayari
wameshateua makampuni mawili ya Ushauri
wa hatua ya kufanya usanifu na maandalizi ya uwekezaji ambapo kampuni ya
Lahmeyer International GmbH ya Ujerumani na Arab Consulting Engineers Moharram –Bakhoum
(ACE) ya Misri ambayo pia ilishiriki
katika kuandaa mchoro wa daraja la
Kigamboni kwa pamoja zitaanza kazi hiyo
march mwaka huu.
Kulingana na maelekezo ya mkataba
kampuni hizo zitatekeleza ushauri huo kwa kipindi cha miaka miwili na kwamba katika kipindi chote nchi mbili za
Malawi na Tanzania zitatoa pia wataalamu
watakaoshirikiana nazo katika utekelezaji na kwamba hatua hiyo ni muhimu katika
kurithisha utaalamu na ujuzi kwaaajili ya uendelezaji wa miradi mingine
baadaye.
Hatua ya kufanya usanifu na maandalizi ya uwekezaji (detailed design
and investment preparation) inatarajiwa kugharimu kiasi cha euro 6,135,515 huku
kiasi kikubwa kikichangiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kupitia mfuko wake wa
Africa Water Facility Special Fund (itachangia euro 3,549,000), wakati NEPAD kupitia mfuko wake wa Miundombinu
itachangia euro 1,226,295 na nchi za
Malawi na Tanzania zitachangia Euro
1,360,220
Kulingana na Meneja wa Program
hiyo Mhandisi Saidi Abbas Faraj mabwawa
ya uzalishaji umeme yatajengwa katika eneo la Mpaka wa wilaya ya Kyela na Ileje
na mengine mawili kwa upande wa Tanzania yatajengwa katika wilaya ya Ileje
wakati kwa upande wa Malawi yatajengwa katika wilaya za Kalonga na Chitipa.
Amesema hatua hiyo licha ya kutoa
fulsa za kiuchumi kwa wananchi wa pande mbili za mpaka wa Malawi na Tanzania
kupitia mto Songwe zikiwemo Kilimo cha umwagiliaji, utalii, ufugaji samaki na uvuvi
na matumizi ya nyumbani pia yatatumika kupunguza maafa kwenye jamii hasa wilaya
ya Kyelana Kalonga ambako mafuriko
yamekuwa yakijitokeza na kuhamisha wananchi kutoka nchi moja na kwenda nyingine
kutokana mto kuhama hama.
Tayari maandalizi ikiwemo ofisi
za menejimenti ya mpango huo zimefunguliwa wilayani kyela ambako utekelezaji
wake wa siku hadi siku utakuwa ukisimamiwa wakati ofisi za bodi zitakuwa Malawi
Mwisho