Adverts

Mar 6, 2013

HUGO CHAVES AFARIKI, MAREKANI ITAMKUMBUKA!

Katika kikao kimojawapo cha Umoja wa Mataifa, alishatoa kali wakati wa utawala wa Bush ambapo akiwa kwenye eneo la kuhutubia akajizugisha kama anapata harufu fulani ya watu waliopita kuhutubia kwenye Cordium hiyo akiwaita mashetani!
"humu ndani kuna harufu imeachwa na mashetani fulani nadhani ni jana  ama juzi walikuwemo humu na ninahisi harufu hiyo bado ipo" akimaanisha viongozi wa mataifa yaliyo tofauti na misimamo ya nchi za kijamaa kama yake.
atakumbukwa kwa jinsi ambavyo alikuwa na misimamo migumu ambayo haikutikisika licha ya vitisho vya hapa na pale vya mataifa kama marekani na ikafikia mahala hadi kutafuta mbinu za kumzima kwa njia ya mbalimbali.
Kuna wadadisi wanaoamini kuwa hata magonjwa ya kansa yaliyomwondoa ni mchakato wa muda mrefu wa kijasusi uliofanikiwa kama ambavyo kiongozi wa Cuba na rafiki mkubwa wa Hugo, Fidery Castrol ambavyo naye ameandamwa na jitihada za kumzamisha kwa muda mrefu hadi hatua ya kumwachia mdogo wake Roul Castrol aongoze taifa hilo
Kalale pema kamanda, mimi niliipenda misimamo yako!, Kimsingi alikuwa mkatoliki mtiifu na  alikuwa akipenda kuibusu Lozari, lakini inapokuja kwenye mitazamo juu ya MAREKANI na mataifa Makubwa yanayopenda kulaza ubabe kwenye nchi zingine wenye maslahi nazo, hapo mzeee huyu alifanana na KOMREDI MUGABE! hakuweza kujishusha na lazima sauti yake isikike!!!
Amefariki jana akiwa na umri wa miaka 58