Timu ya Kimondo SC ya
wilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya imeendelea kutakata katika raundi ya pili
ya ligi ya Mabingwa wa Mikoa baadaya kuisukutua bila dawa timu ya Mji ya Njombe
bao 1-0 juzi katika mchezo uliofanyika uwanja wa sabasaba mjini Njombe
Katika mchezo huo ambao
tangu kuanza kwake ulikuwa ukionyesha jitihada za wazi za kuhitajika mbeleko
kwa timu ya wenyeji, hali iliendelea kuwa tete kadiri dakika zilivyokuwa
zikienda mbele kutokana na mbinu za hapa na pale za mwamuzi kushindwa kupenya
ili kuleta madhara kwa upande wa Kimondo.
Kimondo licha ya majaribio
kadhaa vipyenga vya kuotea vilionekana kuharibu ladha ya mchezo kiasi cha
mashabiki wa Njombe kushindwa uzalendo na kuamua kushabikia timu ya Kimondo
ambayo ilionekana kutandaza soka lenye ladha mithiri ya asali ya Ilomba na
Idiwili.
Katika dakika za mkiani,
baada ya majaribio kadhaa ya kuingia eneo la hatari na kupigiwa vipyenga vya
kuotea, ndipo staili ya “mpime huko huko mbali” ilipoanza na haikuchukua muda
mrefu kwani gonga kama nne kutoka kwenye lango la Kimondo zikielekezwa kwenye
lango la timu ya Mji Njombe ziliwezesha shuti la umbali wa mita 52.56 kuleta sherehe kwa upande wa Kimondo baada ya
kumpima kipa wa Mji Njombe na katika maeneo hatarishi na kusababisha timu
ipumulie mashine mbele ya mashabiki wake uwanja wa nyumbani.
Ushindi huo ulipakatwa kama
mwali na timu ya Kimondo kwani jitihada zote za kujaribu kuondoa aibu uwanja wa
nyumbani kwa Mji Njombe hali iliendelea kuwa ngumu na hadi dakika kumi
zilizoongezwa na mwamzi kumalizika bado Njombe walionekana kuzidiwa pumzi.
Nyongeza ya dakika
ilionekana dhahiri shairi kutaka kusababisha kilio cha bao la pili hivyo mwamzi
akajikuta anapuliza filimbi huku akiangalia huku na kule kuhofia uongozi wa
mkoa uliokuwa upo uwanjani na kushuhudia timu yao ikitoka imetota huku wageni
kutoka Mpakani wakizungumza Kinyiha,Kiwemba,Kinyaki na kinyamwanga huku maneno “Nyinza sana” tununu
fijo”, natemwa, na tukuvifyondomola” yakisikika kwa furaha
Mchezo wa marudiano baina
ya Kimondo SC ya Mbeya na Mji Njombe unatarajiwa kufanyika katika
uwanja wa sokoine mjini Mbeya Jumapili Juni 2 mwaka huu.
Chachandu ya ligi hiyo
inashamihilishwa na namna timu zilivyojipanga kuhakikisha ushindi kwa kufanya
usajiri wa kusugulia meno kwa tupa!!
Nyingine ni Polisi Jamii ya
Bunda mkoani Mara, Biharamulo FC ya Kagera, Saigon FC ya Kigoma na Katavi
Warriors ya Katavi.
Timu zitakazofuzu kucheza
raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati
mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.