Na Danny Tweve Mbozi,
Akizungumza jana kwenye
mkutano wa hadhara ulioambatana na ugawaji
wa madawati kwa shule ya msingi ya Ichenjezya katika mamlaka ya mji wa
Vwawa, Mbunge huyo amesema ingawa hoja hiyo ilionekana kubezwa hatimaye imezaaa
mabadiliko aliyoyafanya mheshimiwa rais kwa kuteua bodi mpya ambayo sasa
itaongozwa na Dr Juma Ngasongwa
Alisema mwaka jana
alimwandikia waziri wa Kilimo Christopher Chiza
kupinga uteuzi uliofanywa na waziri wa Kilimo wakati huo Profesa Jumanne
Maghembe ambapo Dr Eve Hawa Sinare iliteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo huku
wajumbe watano wa kamati hiyo wakitokea
mkoa mmoja.
Katika barua yake ya Juni 4, 2012, Mh Zambi pamoja na kumwandikia waziri wa kilimo
pia alinakili barua hiyo kwa Mh Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akielezea
kukiukwa kwa sheria na utungwaji wa kanuni za zao la kahawa bila kuzingatia
taratibu.
Anasema bodi hiyo ya
awali ilikuwa na wajumbe ambao wengine walikuwa na migongano ya kimaslahi na
wengine kutojulikana makundi wanayowakilisha tofauti na bodi ya sasa ambapo
imehusisha wajumbe kutoka maeneo yote ambayo Kahawa inalimwa.
Anaeleza kuwa
anafurahi kusimama mbele ya wananchi kuwa rais amesikiliza kilio hicho na
kuivunja bodi hiyo pamoja na kuiteua bodi nyingine ambayo sasa inahusisha
maeneo yanayozalisha zao hilo.
“ ninafuraha
kuwaelezeni leo hii kuwa tarehe 30 na 31 mwezi huu wadau wa kahawa watakutana
mkoani Morogoro kuzungumzia maendeleo ya zao la Kahawa mkiwa na bodi mpya
ambayo ina uwakilishi niliokuwa naupigania na kuusimamia” alieleza Mh Zambi.
Amesema katika suala
la kutetea maslahi ya wananchi wake yupo tayari kuitwa vyovyote ilimradi
anasimamia ukweli, na kwamba katika hilo kuna wakati alilaumiwa na kuonekana
akitofautiana na waziri aliyeteuliwa na chama chake, na kwamba alifanya hivyo
kwakuwa anatambua kuwa alikuwa akiwakilisha maslahi ya wapiga kura wake na
wazalishaji wa kahawa nchini kote.
Amesema ni vyema pia
wananchi wake wakatafakari kwa makini kauli iliyokuwa ikisisitizwa na Mbunge wa
awali wa jimbo hilo marehemu Halinga kuwa wananchi wa wilaya hiyo wanapaswa
kuwasomesha watoto wao ili kuepuka kuwa chakula cha wasomi.
Alisema neno hilo si
zuri sana kulizungumzia mbele ya jamii lakini ni ukweli kwamba pasipo kusomesha
watoto wao, wataendelea kuwa watumwa wa jamii iliyosoma ambayo ndiyo yenye
fulsa za kufanya maamuzi huku wao wakiwa watekelezaji tu
Akiwa kwenye mkutano
huo uliofanyika nje ya uwanja wa shule
ya msingi ya Ichenjezya Mh Zambi alitoa msaada wa madawati 100 yenye
thamani ya shilingi Milion sita kwa shule ya Ichenjezya na kufikisha idadi ya
madawati 180 ambayo amekwisha yatoa kwa shule hiyo kwa ushirikiano na mamlaka
ya bomba la mafuta TAZAMA.
MWISHO