MKUU wa wilaya ya Rungwe Bw. Chripin Meela amesema, changamoto zinazokabili sekta ya habari
na vyombo vya habari kwa ujumla ni matokeo ya umuhimu wa taaluma
hiyo katika ukuaji wa demokrasia nchini
Akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa klabu ya wandishi
wa habari mkoa Mbeya unaoendelea ukumbi wa Royal Tughimbe, Mkuu wa wilaya ya
Rungwe Chrispin Meela amesema, wananchi wana matumaini makubwa na vyombo vya
habari na pale kipapota doa la utendaji ni muhimu kujirekebisha kabla ya kutengeza
picha mbaya mbele ya jamii wanayoihudumia
Amesema hali iliyojitokeza hivi karibuni kwenye klabu hiyo
inahitaji kuweka misingi imara ya kiutendaji
na kwamba jitihada za kufanya uchaguzi wakati huu ni hatua muhimu za kuimarisha mfumo
wa kujiwajibisha kama taasisi ya taaluma.
Amesema ikiwa viongozi wa dini na vyombo vya habari
vitajihusisha na ubadhirifu na wizi ni dalili kuwa hakutakuwa na mwingine wa
kukemea jamii itakayokuwa huru na yenye kukemea vita dhidi ya rushwa
Bwana Meela amesema inashangaza kuona hata vyombo vya habari
vinaingia kwenye ufisadi na akaohoji ninani atakayehoji ufisadi serikali na
kwingineko kama nanyi mnaingia kwenye mitego hiyo hiyo?
Katika hatua nyingine amependekeza Vyombo vya habari kujenga utamaduni wa
kujihusisha na ufuatiliaji wa maendeleo vijijini na kwa kufanya hivyo
kutawezesha wananchi kuwasilisha changamoto zinazowakabili kwa watunga sera.
Amesema katika kufikia hilo
ni vyema pia Viongozi wa serikali ngazi za chini kuondoa uoga katika kufanya kazi na vyombo vya habrari na
kwa kufanya hivyo kutasadia kusukuma mbele jitihada za maendeleo
Katika hatua nyingine Bwana Meela amechangia kiasi cha
shilingi 400,000 kwaajili ya uanzishaji wa chama cha kuweka na kukopa cha
wanahabari SACCOS ili kuwezesha kuwapa fulsa wana habari kujisimamia kiuchumi na kupunguza changamoto za kimaisha
zinazowakabili
Katika kufanikisha hilo wanachama wa Mbeya Press club
walijitokeza kuchangishana wenyewe ambapo wamefanikiwa kukusanya mtaji wa papo
kwa papo kiasi cha shilingi 1,400,000/=
Aidha ameshauri klabu ya wandishi wa habari kuwa na ofisi
yake na hvyo kwa kuomba kiwanja kwenye mamlaka za majiji itasaidia kuwapa nguvu
katika kusimamia haki zao wakiwa na uhuru wa kuwekeza kwenye majengo yao.