PICHA ZOTE NA CAPTIONS KWA HISANI YA MWANAFASIHI(MAHIRI WA SIMULIZI BLOG).
|
WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKIPEANA MIKONO NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII, KABLA YA KUANZA KWA MECHI YA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KATIKA UWANJA WA SOKOINE LEO JIONI |
|
TIMU YA POLISI JAMII YA BUNDA-MARA |
|
TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI-MBEYA |
|
GOLIKIPA WA TIMU YA POLISI JAMII EMANUEL DAUD AKISHANGAA GOLI LILILOFUNGWA NA MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO CHARLES HIZA DK YA 12 |
|
GOLI LILIPITILIZA NA KUPENYA KWENYE NYAVU NA KUSABABISHA REFARII NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA MBEYA KUREKEBISHA NYAVU HIZO KWA DAKIKA KADHAA KABLA YA MPIRA HAUJAWEKWA KATI |
|
Add caption |
|
GOLI LA TATU KWA UPANDE WA KIMONDO BAADA YA MPIRA WA PENALT GOLI LILIFUNGWA NA MCHEZAJI LUKA MPOSHI DK 59 |
|
WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKISHANGILIA GOLI |
|
KIPUTE KINAENDELEA UWANJANI |
|
PATASHIKA KATIKA GOLI LA POLISI JAMII |
|
NDEREMO NA HOI HOI ZILITAWALA BAADA YA KIPYENGA CHA MWAMUZI KUPILIZWA HUKU KIMONDO FC IKIWA MBELA KWA MABAO 3-1 |
|
POLISI WALILAZIMIKA KUMTOA NJE YA UWANJA REFARII KUTOKANA NA KUZONGWA NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHEZO |
|
HOI HOI ZA FURAHA ZINAENDELEA |
|
MASHABIKI WAKIWA WAMEMNYANYUA JUU MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK AMBAKISYE BAADA YA TIMU HIYO KUJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU TANZANIA BARA |
|
SHANGWE NA HOI HOI ZINAENDELEA KATIKA DIMBA LA KUMBUKUMBU YA SOKOINE MKOANI MBEYA |
|
KOCHA WA TIMU YA POLIS JAMII MADENGE OMAR AKILALAMIKIA UTARATIBU WA UENDESHAJI WA LIGI HIYO |
|
PONGEZI ZINAENDELEA |
|
'TUMESHINDA TUNAMSHUKURU MUNGU TUMEPITIA VIGINNGI NA VIKWAZO VINGI'' AKIONEKANA ANASEMA MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK MINGA |
|
SHABIKI WA TIMU YA KIMONDO MBEGU MOJA AKIWAZAWADIA WACHEZAJI WA TIMU HIYO SH. 200,000 BAADA YA USHINDI |
Na DannyTweve
Timu ya Kimondo super
sports club ya Mbozi mkoani Mbeya imeungana na ... kuingia daraja la kwanza
Tanzania bara baada ya kumaliza mchezo wake jana kwa kuifunga timu ya Polisi
jamii ya Bunda mkoani mara mabao 3 -1.
Katika mchezo mzuri
na wakasi uliofanyika uwanja wa sokoine jijini Mbeya ulishuhudia Polisi Jamii
wakicheza kufa na kupona licha ya maelezo ya kocha wao kuwa walishtukizwa
mchezo huo kwani TFFA awali walitangaza kuwa ungechezwa siku ya jumapili.
Bao la kwanza la
Kimondo liliwekwa wavuni mnamo dakika ya 12 kupitia kwa Charles Hiza baada ya
kupokea pasi kutoka kwa Geofrey Mlau na kumchungulia mlindamlango wa Polisi
Jamii Emmanuel Daud na hatimaye kumchambua na kuhesabu bao la kwanza
Mashambulizi ya hapa
na pale yaliendelea kwa timu zote ambapo mnamo dakika ya 17 Cosmas Mwazembe wa Kimondo SSC aliunganisha
wavuni kwa kichwa krosi ya Charles Hiza na kuifanya Kimondo kuongeza hamasa kwa
mabao 2 ya haraka haraka waliyoyapata.
Hata hivyo sherehe
hiyo ilidumu kwa dakika 30 tu kwani Polisi jamii kupitia kwa Joseph Onyango
waliweza kuihada ngome ya Kimondo na kuachia shuti kali lililodakwa na kutemwa
kwenye nyavu na kipa wa Kimondo Daud Pius ha hivyo kuwafanya Polisi Jamii
kutoka kipindi cha kwanza wakiwa na matumaini ya kurejesha bao la jingine
katika kipindi cha pili.
Bao la tatu kwa
Kimondo lilifungwa mnamo dakika ya 59
kwa njia ya penati kupitia kwa Lucas Baraka baada ya mshambuliaji
Geofrey Mlau kuangushwa eneo la hatari katika purukushani za kumdhibiti akiwa
njiani kwenda langoni mwao.
Mnamo dakika ya 57 mwalimu
wa Polisi jamii Bunda Madenge Omary
alitolewa eneo la benchi la ufundi baada ya kumtukana mwamuzi wa mchezo huo Daudi Ahadi kutoka
jijini Dar es Salaam na akizungumza
baada ya mchezo huo, alisema wachezaji wake wamechezeshwa wakiwa wamechoka
kutokana na kuwasili asubuhi jijini Mbeya na kulazimishwa kucheza wakati TFF
ilikuwa imetangaza mchezo huo kuchezwa siku ya jumapili na si jumamosi.
Akizungumzia kupanda
daraja kwa timu yao Mkurugenzi wa Timu ya Kimondo Erick Minga ndoto za wilaya ya Mbozi kuwa mkoa
zinakwenda sambamba na ukuzaji wa soka wilayani humo ambapo watahakikisha timu
yao inapanda daraja na kuingia ligi kuu msimu ujao na kuwataka wananchi wa mkoa
wa mbeya kwa ujumla kushiriki katika kuchangia mafanikio ya timu zao.
Alisema tayari sasa
mkoa utakuwa na michezo mfululizo katika uwanja wake wa sokoine kwa kuwa kuna
timu mbili za ligi kuu, pia Kimondo itavuta michezo ya daraja la kwanza hatua
ambayo wananchi watafadi uhondo wa soka mkoani mwao kwa mwaka mzima.