Na Angela Kivavala- Mbozi
Asilimia 44 wakazi wa wilaya ya Mbozi ndiyo wanaopata
huduma ya maaji safi na salama imefahamika
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
mkugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Mbozi Levison Chillewa amesema kwa
sasa wilaya inategemea aina tatu za vyanzo vya maji vikiwemo visima, mitiririko na maji ya chemichemi
zilizo boreshwa.
Akifafanua Chillewa amesema kuna
jumla ya visima virefu na vifupi
105 chemichemi za asili 40 mitiririko 5 na matanki 6 yanayotumika kuvuna maji ya mvua.
Chillewa amesema kupitia
programu ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSR),wilaya inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu
ya maji katika wilaya ya mbozi ambapo hadi sasa visma vitano vinajengwa
ikiwa ni vyanzo vya usambazaji wa maji katika vijiji vitano vya wilaya ya mbozi
Aidha
Kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, halmashauri ya wilaya ya Mbozi imewezesha baadhi ya shule za sekondari
na hususani miradi ya ujenzi wa hosteli
pamoja na baadhi ya huduma kama zahanati na nyumba za walimu kuwa na mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua kwa kuwekewa tanki za plastiki (SIMTANK) zenye ujazo wa
kati ya lita 5000 hadi lita 10,000.
Kuhusiana
na uhifadhi wa mazingira, Mkurugenzi huyo amesema wilaya ya mbozi vyanzo vya 23
tayari vimepimwa na vipo kwenye hatua za kuwekewa alama za kudumu.
aidha halmashauri ya wilaya imeanzisha mfumo
wa kuifadhi takwimu za vyanzo vya maji ambapo hadi mwezi mei jumla
ya vyanzo vya maji 471 vilikuwa vimetambuliwa pia vyanzo vya maji vimepewa
kipaumbele na kamati za maendeleo
za vijiji na kata.
Pamoja na mafanikio wilaya
imekuwa ikikumbanana changamoto mbalimbali ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji
unaotokana na kulima kujenga kuchoma moto na kuchunga mifugo kwenye vyanzo vya
maji na gharama kubwa za uchimbaji na ujenziwa miundombinu ya maji.
Wilaya imeweza kuwekamikkati
ya kuzikabili changamoto hizo ikiwa nipamoja na
kuelimisha jamii kuusu umuhimu wa tuunzaji wa vyanzo vya maji kulinda na
kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchiikiwa ni pamoja na upandaji wa
miti katika vyanzo vya maji, vijiji
vyote vyawilaya vimepewa jukumula kudhibiti uharibifu katika vyanzo vya maji
Kwa mwaka 2013/ 2014
halmashauri imetengewa TSH 1,425,470,049 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo ya maji wilaya ya mbozi
Mwisho