Timu ya Kimondo ya wilayani Mbozi imeendeleza wimbi la
kujitengenezea mazingira mazuri kuingia ligi daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kuilazimisha sare ya
bao 2-2 Timu ya Polisi Jamii ya Musoma katika uwanja wake wa Nyumbabi wa Karume
mjini Msoma
Polisi jamii ambao walianza kupata bao lao la kwanza
walijikuta wakishindwa kubana na badala yake wakaachia mnamo dakika ya 36 baada
ya Kimondo kupanga mashambulizi huku wakiwasiliana kwa kutumia kiwemba, kindali
na kinyiha huku wakiwaaacha maafande wakishangaa hadi Geofrey Mlau akiandika
bao la kwanza na lakusawazisha.
Nyumbani ni nyumbani ilidhihirika baada ya kipindi cha
kwanza kumalizika kwa nguvu sawa kwa kufungana bao moja kwa moja, kipindi cha
pili kilianza kwa mashambulizi ya kasi kutoka polisi jamii ambao waliweza
kupata bao la pili mnamo dakika ya 67 lakini halikudumu muda mrefu kwani mnamo
dakika ya 75 hali ilikuwa mbaya kwa wenyeji
Alikuwa Imani Wilson aliyewainua mashabiki wa Musoma bila
kujali uzalendo kwa timu yao na kuamua kushangilia timu ya wageni Kimondo SC
baada ya kutungua shuti la kufa mtu lililomfanya mlindamlango wa Polisi Jamii
kujifanya kama vile alikuwa akisikiliza simu kwa jinsi lilivyoingia na
kumchanganya kabisaa.
Ikiongozwa na mlezi wao ERICK MINGA Kimondo iliendelea
kufanya mashambulizi yenye lengo la kuwadharirisha wenyeji kwenye uwanja wao wa
nyumbani hata hivyo mashambulizi hayo yaliiishia kwa kosa kosa, hadi timu
inatoka uwanjani wananchi wa Musoma walishindwa kuvunga na badala yake
wakajikuta wakitoa mikono ya pongezi kwa mtanange mtamu ulioonyeshwa na Kimondo
Sc.
Katika kudhihirisha nia ya kupata mkoa mpya wa Songwe,
Wilaya ya Mbozi kupitia wadau wake imeendelea kusukuma mbele ajenda ya michezo
ambapo miongoni mwa wadau FULL DOSE ambaye amejitokeza mbele kuidhamini timu
hiyo anaeleza kuwa tutaingia mkoa mpya tukiwa na timu mpya ya ligi kuu!!
|