Na Angela kivavala
Halmashauri
ya wilaya Mbozi ina kabiliwa na tatizo la ukosefu wa shule za sekondari za kidato cha tano na sita.
Wilaya
ina jumla ya shule za sekondari 55 ambazo kati ya hizo 40 ni za serikali na 15
ni za binafsi.kati ya shule hizo ni sita tu zenye elimu ya kidato cha tano na
sita ambapo ya serikali ni moja nane za watu binafsi.
Kutokana
na hali hiyo watoto wanaohitimu kidato cha nne wanalazimika kwenda nje ya
wilaya ya Mbozi hususani katika jiji la
Mbeya kujiunga na kidato cha tano hali ambayo inawaingiza kwenye gharama kubwa
wazazi wao
Aidha
changamoto nyngine ni kasi ya ongezeko la watu ambapo ni matokeo ya kuzaliana
kwa kasi ambapo kulingana na takwimu za sensa ya mwaka 2012, Mbozi ina jumla ya
wakazi 446,339 na kati yake 55% wakiwa
ni vijana na watoto.
Kwa
mwaka wa fedha 2012/2013 hadi kufikia Januari, 2013 jumla ya vyumba vya madarasa 11
vilijengwa katika shule 4 zilizopo Wilayani Mbozi na vyumba vyote vilikuwa vimekamilika na kupokea
wanafunzi 398 waliofaulu ambayo ni sawa na asilimia 100 ya wanafunzi waliokuwa
wamekosa nafasi.
Wilaya
ina shule za msingi 160 ambazo kati ya hizo 158 sawa na 99% zinamilikiwa na
Serikali na shule mbili (2) ni za watu binafsi.
Shule hizo zina jumla ya wanafunzi 93,516, ambao 45,789 sawa na 49% ni
wavulana na 47,727 sawa na 51% ni wasichana.
Aidha shule hizo zina jumla ya walimu 2,000
Changamoto zinazo ikumba sekta hii ya elimu ni
pamoja na upungufu wa walimu 464 kati ya
mahitaji ya walimu 2,564 na kuwa na shule moja tu yenye kidato cha tano na sita ya serikali na shule moja ya binafsi.
Kwa
upande wa Sera ya Afya ya Tanzania inataka kila kijiji kuwa na zahanati. Wananchi wamejenga zahanati 20 ambazo zipo
hatua mbali mbali za ujenzi na 3 zimekamilika na zimeanza kutumika mwezi
Januari 2013.
Hivyo, jumla ya vijiji
vyenye zahati hadi sasa ni 72 kati ya vijiji 101 vilivyopo katika Wilaya ya
Mbozi ifikapo 2015 takribani vijiji 82 vitakuwa na zahanati.
Kulingana
na taarifa iliyotolewa kwenye maadhimisho ya serikali za mitaa wilayani humo ,Sekta ya afya ina changamoto
ya upungufu wa wafanyakazi na vitendeakazi vikiwemo vifaa tiba pamoja na watoa huduma kwa
ujumla.
Hayo
yalisemwa katika taarifa ya utendaji ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa wananchi wa wilaya ya Mbozi katika maadhimisho ya siku ya selikari za mitaa yakiwa na lengo la kutoa mwanya kwa jamii
kutambua na kuzifahamu shughuli za huduma mbali mbali zinatolewa na Taasisi za
Serikali za Mitaa yaani Halmashauri Majiji, Manispaa na za wilaya.
Mafanikio
hayo yametokana na Kuhamasisha na kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika
ujenzi wa madarasa, ushiriki wao ulitoa mchango mkubwa katika kufanikisha zoezi
hiliMshikamano wa viongozi wakuu wa Serikali na halmashauri katika wilaya
kufuatilia, kusimamia na hususani waheshimiwa madiwani.