Baraza la Madiwani la Wilaya ya Mbozi limeombwa kushiriki katika kukemea matukio ya
mauaji yaliyoanza kuibuka ambapo kwa mwezi
September peke yake kumekuwa na matukio
matano.
Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani la wilaya
hiyo Mkuu wa wilaya Mbozi Dr Michael Kadeghe amesema hali hiyo inakwamisha
jitihada za kuvutia kwenye fulsa mbalimbali zilizopo kwa kujenga hofu kwa
wageni
Amesema pamoja na matukio ya mauaji, pia matukio ya
ushirikina katka kipindi hicho hicho yameripotiwa matukio saba
Akifafanua alisema katika kijiji cha Itaka mmoja wa
watuhumiwa wa ushirikina alipohijiwa kama anajihusisha na mambo hayo alikiri
kuyafanya kwa kutumia “majini”
Inaelezwa na mkuu huyo
wa wilaya kuwa katika kujaribu kupata uhakika wa anachokifanya bwana huyo,
alimtaka washindane naye ambapo jamaa alianza kupandisha maruhani yake ili
amfanyie uchawi Dc hali ambayo bwana
Kadeghe alilazimika kumzima kwa kumzuia asiendelee
Huku madiwani wakicheka kwenye kikao hicho, Dc alisema kama
huyu jamaa alikuwa tayari kufanya ushirikina mbele ya kamati ya ulinzi na
usalama unadhani wananchi wa kawaida huko chini hali inakuwaje?
Alisema katika hatua nyingine kumekuwepo matukio ya mara kwa
mara ya wanavijiji kuwafukuza watu wanaotuhumiwa kufanya ushrikina vijijini na
kwamba katika matukio ya hivi karibuni walimwokoa mwanamke mmoja aliyekuwa
aliyetuhumiwa katika kata ya Nambinzo.
Alisema kasi ya wanavijiji kuwahamisha watuhumiwa wa vitendo
vya kishirikina wilayani humo vinaashiria kuwa matukio ya imani hizo
yamewachosha na yanaweza kusababisha kutoweka kwa amani kwenye jamii.
Alisema yeye hana uwezo wa kuhamisha watu kwenye vijiji na
mamlaka hayo anayo mheshimiwa rais pekee hivyo kumekuwa na ugumu kufanya
maamuzi ya namna hiyo licha ya viashiria vya ushirikina katika jamii kuoneka.