Na Mwandishi wa Indabaafrica
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Mh Mlugo
ameagiza uongozi wa shule ya sekondari ya Holly Wood ya wilayani Mbozi
kuwasomesha wanafunzi 69 wa kidato cha pili waliozuiwa na uongozi wa shule hiyo
kufanya mitihani ya kuingia kidato cha
tatu
Katika uamuzi huo alioutoa juzi, Baraza la Madiwani Mbozi
limeelezwa kuwa sambamba na hilo, uongozi wa shule hiyo pia umepewa kalipio kwa
maamuzi yake kinyume na maelekezo ya wizara hiyo.
BAADHI YA MADIWANI NA WATAALAMU WAKIFUATILIA KIKAO HICHO, WA KWANZA MBELE NI MH SAMWEL MTAWA ALIYEIBUKA NA SWALI LA PAPO KWA PAPO KUHUSIANA NA WANAFUNZI WA HOLLYWOOD WALIOZUIWA KUFANYA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI
MADIWANI WAKIWA WANAFUATILIA MICHANGO UKUMBINI
MWENYEKITI WA HALMASHAURI KATIKATI NA KOFIA AKIWA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA CCM KUSHOTO KWAKE NA KULIA KWAKE NI KAIMU MKURUGENZI NA MKUU WA WILAYA ALIYESIMAMA
MWENYEKITI WA HALMASHAURI MH ERICK AMBAKISYE MINGA NA KAIMU MKURUGENZI DR CHARLES MKOMBACHEPA
Katika maswali ya papo kwa papo kwenye baraza la madiwani ,
Diwani wa kata ya Isandula Samwel Mtawa alimuuliza mwenyekiti wa halmashauri hatua
zilizochukuliwa kuwasaidia watoto 69 waliozuiwa kufanya mitihani ya kidato cha
pili kutokana na kasoro za kutofikia wastani uliowekwa na shule hiyo kwenye
mitihani ya MOCK na majaribio.
Akijibu swali hilo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alisema,
Mheshimiwa waziri amepokea malalamiko hayo na kuwasiliana na kamishna wa elimu
ambapo ilishindikana kufanywa upya mitihani hiyo kwa mwaka huu, na ikaelekezwa
mitihani hiyo kufanywa mwakani.
Naye mkuu wa wilaya ya Mbozi Dr Michael Kadeghe alitoa
ufafanuzi wa suala hilo alisema kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ilipokea
taarifa za uongozi wa shule hiyo kuwazuia wanafunzi 70 kufanya mitihani ya
kidato cha Pili nailifikiwa maamuzi kwa shule hiyo kuzuiwa kupokea wanafunzi wa
kidato cha kwanza kwa mwaka 2013/2014
Akitoa maelezo ya adhabu iliyotolewa na waziri Mlugo, mkuu
huyo wa wilaya alisema waziri aliagiza uongozi wa shule hiyo kuwaghalimia
wanafunzi hayo ada ya mwaka mmoja pamoja na mahitaji mengine ya shuleni hadi
watakapofanya mtihani wao wa kuingia kidato cha tatu mwakani.
Aidha imeelezwa kuwa uongozi wa shule hiyo pia uliagizwa
kughalimia ada za wanafunzi hao watakaoamua kuhamia shule nyingine kwa kipindi
cha mwaka mmoja bila kujali gharama za shule hizo wanazokwenda.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amekemea tabia
iliyozuka kwa shule za sekondari binafsi kuweka utaratibu wa kuchuja wanafunzi
kutokana na ufaulu wa mitihani ya ndani kwa lengo la kufanya mashindano ili
zionekane shule hizo ni bora kitaifa.
Alisema wakuu wa shule hizo wanapaswa kuonyesha uwezo wao kwa
kuwafundisha wanafunzi hadi kufaulu na siyo kuchuja wale wanaoshindwa kwenye
mitihani ya majaribio na baadaye kuwafukuza kwenye shule zao.