KATIBU WA MUDA WA TFF BONIFACE WAMBURA
Tanzania Football
Federation
Affiliated to FIFA,
CAF and CECAFA
Karume Memorial
Stadium, Uhuru/Shaurimoyo RoadP.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania
.
Telefax: + 255-22-2861815E-mail:tanfootball@tff.or.tz
Website:www.tff.or.tz
Release No.
194TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARINovemba 12, 2013
BODI YA LIGI YAFUNGIA VIWANJA SABA
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board)
imefungia viwanja saba vilivyokuwavikitumiwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) na Ligi Daraja la Kwanza(FDL) hadi vitakapofanyiwa marekebisho ili
kukidhi mahitaji ya mechi zampira wa miguu.Uamuzi huo umefikiwa na TPL
Board katika kikao chake cha kwanzakilichofanyika juzi (Novemba 10 mwaka
huu) jijini Dar es Salaam ambapopamoja na mambo mengine kilipitia ripoti za
mechi za VPL na FDL katikamzunguko wa kwanza.
Viwanja vilivyofungiwa na marekebisho
yanayotakiwa kufanyika kwanza iliviruhusiwe kutumika tena ni Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba (majukwaa yakeyamechakaa, hivyo kuhatarisha usalama wa
watazamaji), na Uwanja wa CCMMkwakwani jijini Tanga (vyumba vya wachezaji kubadilishia
nguo (dressingrooms) havina hadhi).Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya
(sehemu ya kuchezea- pitchni mbovu), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri
Abeid jijini Arusha(pitch ni mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya
kubadilishiakutumika kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji
mjini Songea(pitch ni mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni
mbovu).
Klabu ambazo timu zake zinatumia
viwanja hivyo zimeshaarifiwa rasmi juu yauamuzi huo ambapo ama vinatakiwa
kuwasiliana na wamiliki wa viwanja hivyoili wafanye marekebisho au kutafuta
viwanja vingine vya kuchezea mechi zao.Kwa upande wa ripoti za mechi za VPL;
Mbeya City imepigwa faini ya sh.500,000 na kupewa onyo kali kwa timu yake ya
U20 kutocheza mechi yautangulizi walipocheza na Yanga. Pia wanatakiwa kulipa
gharama za uharibifubaada ya washabiki wao kuvunja kioo cha basi la Yanga baada
ya gharamahizo kuthibitishwa na Bodi ya Ligi.
Pia Mbeya City imepigwa faini ya sh.
500,000 kwa washabiki wakekushambulia basi la wachezaji wa Tanzania Prisons
baada ya mechi dhidi yao,na kulipa gharama za uharibifu baada ya kuthibitisha
na Bodi ya Ligi.Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu
za washabikiwake ilipocheza na Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo
mwamuzimsaidizi Hassan Zani alishambuliwa kwa mawe na kujeruhiwa mkononi
nakichwa, tukio lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika tatu.Beki wa Coastal
Union, Hamad Khamis wa Coastal Union amepigwa faini ya sh.500,000 kwa
kumpiga kichwa kwa makusudi Kipre Tchetche wa Azam.
Kitendo hicho kilisababisha refa amtoe
nje kwa kadi nyekundu, hivyo atakosa mechitatu zinazofuata za timu
yake.Mchezaji Cosmas Lewis wa Ruvu Shooting alifanya kitendo cha utovu
wanidhamu kwa kupiga kelele wakati mgeni rasmi akisalimia timu na
kukataakupeana mkono na kamishna kwenye mechi dhidi ya Rhino Rangers,
hivyoamefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000.Mtunza vifaa (Kit
Man) wa JKT Ruvu, Selemani Oga aliondolewa kwenyebenchi la ufundi wakati
wa mechi yao dhidi ya Mbeya City kwa kosa la kutoalugha chafu kwa refa,
hivyo suala lake litapelekwa katika Kamati ya Maadili.Kocha Msaidizi wa
Oljoro JKT, Fikiri Elias amepigwa faini ya sh. 500,000 nakufungiwa mechi tatu
kwa kumshambulia kwa matusi refa wakati wa mechiyao dhidi ya Ashanti
United.
Naye mtunza vifaa wa timu hiyo Elas
Justinamepele kwa Kamati ya Maadili kwa kumshambulia refa kwa matusi ya
nguoni.Simba wamepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za
washabiki wakewakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.Katika FDL, mchezaji Ally
Mtoni wa Villa Squad amepigwa faini y ash. 200,000na kufungiwa mechi tano.
Kosa lake ni kujisaidia haja ndogo golini wakti wamechi dhidi ya Ndanda FC
iliyochezwa mjini Mtwara.
Kamishna Paul Opiyo wa mechi ya FDL
kati ya Villa Squad na Transit Campkwa kutokuwa makini. Katika ripoti yake
ameeleza kuwa Transit Campilichelewa kufika uwanjani, lakini hakusema
ilichelewa kwa muda gani.Kocha wa Polisi Dar es Salaam, Ngelo Nyanjabha na
Meneja wa timu hiyoMrimi Masi wamepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa
mechi tatu kilammoja kwa kuongoza kundi la washabiki kumvamia refa wa mechi yao dhidiya
Villa Squad iliyochezwa Dar es Salaam.
Pia Bodi ya Ligi imeagiza Polisi
waandikiwe barua ya onyo kwa vile wakatiwaamuzi wanapigwa walikuwepo lakini
hawakutoa msaada kwa wakati.Kocha wa Friends Rangers, Kheri Mzozo amepigwa
faini ya sh. 200,000 nakufungiwa mechi sita kwa kosa la kumtukana refa na
kutishia kuhamamishawashabiki waingie uwanjani kufanya fujo kwenye mechi dhidi
ya Villa Squad.Naye Kocha msaidizi wa timu ya Transit Camp, Haji Amiri
amepigwa faini yash. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kutoa lugha ya matusi
kwa mwamuziwa akida wakati wa mechi dhidi ya Friends Rangers.Adhabu zote
zimetolewa kwa mujibu wa kanuni.
Pia Bodi ya Ligi imeahirishakufanya
uamuzi wa mechi kati ya Stand United na Kanembwa JKT iliyochezwaUwanja wa
Kambarage ili kukusanya taarifa zaidi. Mechi hiyo haikumalizika.Bodi ya Ligi
itakutana tena Jumapili (Novemba 17 mwaka huu).
FUTURE TAIFA
STARS vs TAIFA STARS UWANJANI KARUME
Timu za Taifa za Future Taifa Stars na Taifa Stars zinacheza kesho
(Novemba13 mwaka huu). Mechi hiyo ya kirafiki itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu
yaKarume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.Mechi hiyo ni maalumu
kwa Benchi la Ufundi la Taifa Stars linaloongozwa naKim Poulsen kuangalia
wachezaji kumi kutoka Future Taifa Starswatakaoongezwa katika Taifa Stars
tayari kwa mechi ya kirafiki ya kimataifaitakayochezwa Novemba 19 mwaka huu
jijini Arusha.Watazamaji 300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo kwa
kiingilio cha sh.5,000.