Dec 10, 2013

SIMANZI- DIWANI WA VITI MAALUM CCM -KATA YA ITAKA MBOZI HATUNAYE TENA

Enzi za maisha yake Mh Diwani Salome Lazaro Kibweja akiwa katika moja ya vikao vya baraza la madiwani Mbozi

Baadhi ya waliomfahamu Mh Kibweja wakishindwa kujizuia kulia katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi leo asubuhi 

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Mbozi Erick Minga akizungumza na menejiment ya halmashauri ya wilaya katikati ni afisa Utumishi na raslimali watu bwana Lulandala na kushoto ni Dr Mkombachepa mkurugenzi wa halmashauri hiyo

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dr Charles Mkombachepa akizungumza kwa ufupi namna ratiba ya mazishi itakavyokuwa


Baadhi ya waheshimiwa madiwani wakiwa wametulia ukumbini kabla ya kuanza kuaga mwili wa marehemu

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Mh Erick Minga akitoa taarifa ya msiba huo, sambamba na kusoma historia ya marehemu Salome Kibweja 


Afisa Usafirishaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Paschal Chuwa akitoa ufafanuzi kwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Erick Minga kabla ya kuanza safari ya kuuepeleka mwili wa marehemu kijiji cha Itaka kwaajili ya Mazishi


Na Danny Tweve-Mbozi
Aliyekuwa diwani wa viti maalumu wa kata ya Itaka -Salome Lazaro Kibweja ameagwa rasmi na watumishi na waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi leo asubuhi tayari kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika mchana huu kijijini kwake Itaka.

Salome alifariki usiku wa kuamkia 8 decemba katika hospitali ya rufaa ya Mbeya baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa anashiriki sherehe ya kipaimara ya mtoto wa dadayake jijini Mbeya

Salome Kibweja aambaye alizaliwa mwaka 1975 alihitimu darasa la saba 1991 na akaingia kwenye siasa na kugombea viti maalumu mwaka 2010 ambako alishinda viti maalumu.

kulingana na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Minga, akiwa kwenye sherehe hiyo siku ya jumamosi Disemba 7 alianza kujisikia kuumwa kichwa ambapo alipelekwa kwenye zahanati ya jirani na eneo la sherehe na baadaye kufikishwa hospitali ya rufaa ya Mbeya.

Mazishi ya Mheshimiwa Kibweja yatafanyika katika kijiji cha Itaka leo mchana 


Nov 15, 2013

OFISI YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA UMASKINI WA CHAKULA, VIJIJINI HALI NI MBAYA ZAIDI KULIKO MIJINI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU  MATOKEO YA  UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI (HBS) TANZANIA BARA 2011/12, TAREHE 14 NOVEMBA, 2013

Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wizara ya Fedha iliendesha Utafiti wa Mapato na Matumizi ya  Kaya Binafsi Tanzania Bara katika mwaka 2011/12. Utafiti huu  ulikusanya, kuandaa na kuchambua taarifa za mapato, matumizi na manunuzi ya kaya

Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka 2011/12 umelenga kutoa  viashiria vitakavyosaidia kufuatilia na kutathmini maendeleo ya  sekta mbalimbali zilizoainishwa kwenye  Mkakati wa Kukuza  Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) Tanzania.
Takwimu zilizokusanywa zilihusu watu na kaya katika maeneo  yafuatayo:
 Elimu na afya ya Wanakaya;
 Manunuzi na matumizi ya kaya;
 Umiliki wa vifaa na rasilimali;
 Makazi na vifaa vya ujenzi;
 Upatikanaji wa huduma na vifaa;
 Upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira;
 Shughuli za kiuchumi na ajira;
 Utalii;
 Umiliki wa biashara zisizo za kilimo; na
 Shughuli za kilimo.
Utafiti huu ulifanyika kuanzia mwezi
Oktoba 2011 hadi Oktoba 2012 ambapo jumla ya kaya  10,186  kati ya 10,400 zilizokuwa zimelengwa zilihojiwa  kutoka katika maeneo ya Dar es Salaam, maeneo mengine  ya mjini na vijijini, Tanzania Bara.

Kila kaya iliyochaguliwa  ilihojiwa juu ya masuala yote yaliyotajwa hapo juu pamoja na  kujaza  kijitabu  cha kumbukumbu  ambacho kaya  ilitakiwa kuandika  mapato na matumizi ya kila siku kwa  muda wa siku 28 mfululizo. Kijitabu hiki cha kumbukumbu  kililenga katika kupata matumizi ya moja kwa moja (hasa chakula)  ya kaya pamoja na matumizi mengine yasiyo ya  chakula kwa kipindi hicho cha siku 28.

Matokeo  ya utafiti huu yanaonesha  kuwa  kiwango cha umaskini wa chakula na ule wa mahitaji ya msingi  ni tatizo zaidi kwa  Wananchi wa vijijini ikilinganishwa na Wananchi wanaoishi mjini hususan Dar es Salaam na maeneo mengine ya mjini. Wakati wastani wa kitaifa wa kiwango cha umaskini  wa chakula ni asilimia  9.7,  kiwango hicho kinafikia  asilimia 11.3 kwa maeneo ya vijijini.

Dar es Salaam ina  kiwango cha chini kabisa cha umaskini wa chakula cha asilimia  1.0 ambapo  Wananchi  anaoishi maeneo mengine ya mjini wana umaskini wa chakula wa asilimia 8.7.
Kwa upande wa umaskini wa mahitaji ya msingi, wastani wa  Tanzania Bara ni asilimia 28.2  kilinganishwa na asilimia 33.3  kwa maeneo ya vijijini na asilimia 21.7 kwa maeneo mengine  ya mjini. Dar es Salaam ina kiwango cha chini cha umaskini wa  mahitaji ya msingi cha asilimia 4.1.

Matokeo ya utafiti huu yanaonesha  jitihada za Serikali katika kuongeza ujenzi wa shule zaidi hasa
zile za sekondari ambazo zimewezesha kupanda kwa kiwango  cha wanafunzi wanaojiunga katika elimu ya sekondari  kwa  karibu mara mbili, kutoka asilimia 15 mwaka 2007 hadi  asilimia 29 mwaka 2011/12.


Matumizi ya nishati ya umeme katika maisha ya kila siku ya  Wananchi katika kaya ni eneo lingine ambalo Serikali imelenga kuliboresha katika jitahada zake za kuboresha maisha ya  Wananchi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha  kuwa  kaya zinazotumia umeme angalau kwa ajili ya mwangaza wa ndani  zimeongezeka kutoka asilimia 13  kwa mwaka 2007 hadi asilimia 18 kwa mwaka 2011/12

Nov 14, 2013

WAZIRI WA TAMISEMI ASEMA HAHAMISHI WATUMISHI MBOZI!

 Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya pamoja na watumishi wakifuatilia kikao hicho
 Baadhi ya watumishi na madiwani wakifuatilia kikao hicho
 Madiwani wakiwa na watumishi kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi
 Waziri Ghasia akizungumza na watumishi na madiwani 
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mh Hawa Ghasia amesema hatahamisha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa sasa mpaka baada ya kutolewa kwa taarifa ya ukaguzi maalumu uliofanywa na Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali.

Akijibu ombi la Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi aliyemtaka waziri kufanya mabadiliko makubwa kwa wakuu wa idara wa Halmashauri hiyo kwa kile alichokiita kukosekana kwa uwajibikaji huku akimshambulia moja kwa moja Mkurugenzi wake anayestaafu Bwana Levision Chilewa kuwa yeye na wakuu wake wa idara hawakuwajibika na kuisababishia hasara halmashauri hiyo.

Ingawa Mkurugenzi Mtendaji aliyekuwa anasemwa kikaoni hapo hakuwepo, Mbunge huyo aliendelea kumtaja kuwa hata kama angekuwepo angempa hayo hayo kuwa alimjibu waziri wa nchi  ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia sera na uratibu Mh Lukuvi alipokuja wilayani Mbozi "majibu ya kitoto" kuhusiana na kwanini wilaya ya Mbozi ilipata hati ya mashaka mwaka 2011/2012.


Akizungumzia suala la kuwahamisha watumishi hao kama lilivyoombwa na mbunge Zambi, Waziri Ghasia alisema maamuzi ya watumishi walio chini ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya yapo chini ya Madiwani ambao Mbunge ni sehemu yake

Alisema yeye hata hamisha mtu wakati huu ambapo taarifa ya Ukaguzi maalumu kwa wilaya hiyo haujatolewa na akawataka watumie mamlaka yaliyo ndani yao katika kushughulikia masuala ya nidhamu na utendaji wa watumishi badala ya kusubiria TAMISEMI itekeleze hata kwenye maeneo ambayo wana uwezo nayo.

Waziri Ghasia amesema " ukiachilia Mkurugenzi mtendaji wengine wote ni mali ya halmashauri ya wilaya husika na hawa wanaokaimu nafasi mbalimbali wanapaswa kuthibitishwa na halmashauri za wilaya husika sana sana mnaweza kutuomba TAMISEMI tuwasaidie kuwafanyia upekuzi kabla hawajapandishwa vyeo lakini suala la mapendekezo linatoka kwenu.
 Kikao hicho pia kimezungumzia suala la mgawanyo wa mkoa wa Mbeya na kupata Mkoa wa Momba ambapo waziri Ghasia amesema, yeye pia alipewa maelekezo na Mh Waziri mkuu kufuatilia suala hilo na kwamba hatua ya kwanza amewaagiza wilaya ya Chunya kuomba kugawanywa na kuwa wilaya  Mbili kutokana na ukubwa wa eneo la wilaya hiyo.

hata hivyo amesema suala la kugawanya mkoa huo hataweza kulizungumzia kwakuwa linachangamoto nyingi na kwamba litazungumzwa na waheshimiwa wabunge na ikiwezekana maamuzi yataweza kutolewa baada ya mazungumzo hayo.

Kuhusiana na kuigawa wilaya ya Mbozi na kuwa na halmashauri nyingine, waziri Ghasia alisema wilaya inaweza kuanzisha mchakato huo na kuwasilisha mapendekezo hayoofisini kwake naye ataangalia vigezo katika kufikia maamuzi, tofauti na wilaya ya Chunya ambayo amesema kulingana na ukubwa wa eneo lake ambalo  linafikia kilometa za mraba 29,000 ambayo ni zaidi ya baadhi ya mikoa hapa nchini amelazimika kutoa maamuzi ya papo kwa papo ili waendelee na mchakato wa kugawa wilaya hiyo
 Katika hatua nyingine waziri huyo ametangaza hatua ya kurejesha kwenye ngazi za wilaya baadhi ya ajira za kada za chini baada ya apendekezo yaliyopelekwa kwa mheshimiwa Raisi kusainiwa katka mabadiliko ya utaratibu wa ajira za umma

Alisema kada za chini zitaanza kufanyiwa ajira kwenye wilaya husika lakini, wilaya zisubiri maelekezo ambayo yapo mbioni kutolewa hivi karibuni

Kuhusiana na marekebisho ya mishahara na upandishaji madaraja, waziri amesema serikali tangu iondoe madaraka ya kupandisha na kufanya marekebisho ya mishahara ya watumishi kwenye mfumo wa Lawson, Malalamiko ya muda mrefu ya kucheleweshewa malimbikizo na kutopandishwa madaraka kwa wakati yamemalizika.
Alisema kwa sasa ikitokea kucheleweshwa kwa mtu kupandishwa daraja ama kurekebishiwa mshahara basi ajue ni kutokana na kutowasilisha viambatanisho vyake vikiwemo vyeti . Aidha alisema malimbikizo ya mishahara ya watumishi yatakuwa yamelipwa yote ifikapo 2015.
MADIWANI WANAPEWA PASU NA WATUMISHI!
Katika hatua nyingine amewashambulia madiwani kuwa baadhi yao wamekuwa wakipewa fedha , kugawiwa kilo 3 za sukari na hata kupewa lift ili wapunguze makali ya kuwashambulia watumishi na badala yake wanakuwa wapole wakishapewa ofa hizo.
Akitolea mfano wa sehemu nyingine alisema kuna madiwani wakipewa lifti ya gari hadi kwao, kesho yake wakirejea kwenye vikao vya halmashauri wanakuwa watetezi wa watumishi waliowapa lifti!

Alisema hali hiyo inawadhalilisha madiwani na kuwaondolea uhalali wakusimamia masuala ya maendeleo.

Katika hatua nyingine Mh Waziri amesema kanuni mpya za madiwani zimeruhusu kamati zote za kudumu za halmashauri kushiriki kwenye ukaguzi wa miradi ya Maendeleo ambapo zitaanza kutekelezwa mara zitakapofikishwa wilayani.

Alisema sambamba na hilo Kamati ya fedha itaongezwa wajumbe na hasa kwa halmashauri zenye baraza kubwa la madiwani.

Nov 12, 2013

VIWANJA SABA VYA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA VYAFUNGIWA


KATIBU WA MUDA WA TFF  BONIFACE WAMBURA 

Tanzania Football Federation
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA
Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shaurimoyo RoadP.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania
.
 Telefax: + 255-22-2861815E-mail:tanfootball@tff.or.tz
 Website:www.tff.or.tz 

 Release No. 194TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARINovemba 12, 2013

BODI YA LIGI YAFUNGIA VIWANJA SABA
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) imefungia viwanja saba vilivyokuwavikitumiwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza(FDL) hadi vitakapofanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya mechi zampira wa miguu.Uamuzi huo umefikiwa na TPL Board katika kikao chake cha kwanzakilichofanyika juzi (Novemba 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam ambapopamoja na mambo mengine kilipitia ripoti za mechi za VPL na FDL katikamzunguko wa kwanza.

Viwanja vilivyofungiwa na marekebisho yanayotakiwa kufanyika kwanza iliviruhusiwe kutumika tena ni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba (majukwaa yakeyamechakaa, hivyo kuhatarisha usalama wa watazamaji), na Uwanja wa CCMMkwakwani jijini Tanga (vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo (dressingrooms) havina hadhi).Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya (sehemu ya kuchezea- pitchni mbovu), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha(pitch ni mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya kubadilishiakutumika kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji mjini Songea(pitch ni mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni mbovu).

Klabu ambazo timu zake zinatumia viwanja hivyo zimeshaarifiwa rasmi juu yauamuzi huo ambapo ama vinatakiwa kuwasiliana na wamiliki wa viwanja hivyoili wafanye marekebisho au kutafuta viwanja vingine vya kuchezea mechi zao.Kwa upande wa ripoti za mechi za VPL; Mbeya City imepigwa faini ya sh.500,000 na kupewa onyo kali kwa timu yake ya U20 kutocheza mechi yautangulizi walipocheza na Yanga. Pia wanatakiwa kulipa gharama za uharibifubaada ya washabiki wao kuvunja kioo cha basi la Yanga baada ya gharamahizo kuthibitishwa na Bodi ya Ligi.

Pia Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wakekushambulia basi la wachezaji wa Tanzania Prisons baada ya mechi dhidi yao,na kulipa gharama za uharibifu baada ya kuthibitisha na Bodi ya Ligi.Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabikiwake ilipocheza na Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo mwamuzimsaidizi Hassan Zani alishambuliwa kwa mawe na kujeruhiwa mkononi nakichwa, tukio lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika tatu.Beki wa Coastal Union, Hamad Khamis wa Coastal Union amepigwa faini ya sh.500,000 kwa kumpiga kichwa kwa makusudi Kipre Tchetche wa Azam.

Kitendo hicho kilisababisha refa amtoe nje kwa kadi nyekundu, hivyo atakosa mechitatu zinazofuata za timu yake.Mchezaji Cosmas Lewis wa Ruvu Shooting alifanya kitendo cha utovu wanidhamu kwa kupiga kelele wakati mgeni rasmi akisalimia timu na kukataakupeana mkono na kamishna kwenye mechi dhidi ya Rhino Rangers, hivyoamefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000.Mtunza vifaa (Kit Man) wa JKT Ruvu, Selemani Oga aliondolewa kwenyebenchi la ufundi wakati wa mechi yao dhidi ya Mbeya City kwa kosa la kutoalugha chafu kwa refa, hivyo suala lake litapelekwa katika Kamati ya Maadili.Kocha Msaidizi wa Oljoro JKT, Fikiri Elias amepigwa faini ya sh. 500,000 nakufungiwa mechi tatu kwa kumshambulia kwa matusi refa wakati wa mechiyao dhidi ya Ashanti United.

Naye mtunza vifaa wa timu hiyo Elas Justinamepele kwa Kamati ya Maadili kwa kumshambulia refa kwa matusi ya nguoni.Simba wamepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wakewakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.Katika FDL, mchezaji Ally Mtoni wa Villa Squad amepigwa faini y ash. 200,000na kufungiwa mechi tano. Kosa lake ni kujisaidia haja ndogo golini wakti wamechi dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa mjini Mtwara.

Kamishna Paul Opiyo wa mechi ya FDL kati ya Villa Squad na Transit Campkwa kutokuwa makini. Katika ripoti yake ameeleza kuwa Transit Campilichelewa kufika uwanjani, lakini hakusema ilichelewa kwa muda gani.Kocha wa Polisi Dar es Salaam, Ngelo Nyanjabha na Meneja wa timu hiyoMrimi Masi wamepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi tatu kilammoja kwa kuongoza kundi la washabiki kumvamia refa wa mechi yao dhidiya Villa Squad iliyochezwa Dar es Salaam.

Pia Bodi ya Ligi imeagiza Polisi waandikiwe barua ya onyo kwa vile wakatiwaamuzi wanapigwa walikuwepo lakini hawakutoa msaada kwa wakati.Kocha wa Friends Rangers, Kheri Mzozo amepigwa faini ya sh. 200,000 nakufungiwa mechi sita kwa kosa la kumtukana refa na kutishia kuhamamishawashabiki waingie uwanjani kufanya fujo kwenye mechi dhidi ya Villa Squad.Naye Kocha msaidizi wa timu ya Transit Camp, Haji Amiri amepigwa faini yash. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kutoa lugha ya matusi kwa mwamuziwa akida wakati wa mechi dhidi ya Friends Rangers.Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa kanuni.

Pia Bodi ya Ligi imeahirishakufanya uamuzi wa mechi kati ya Stand United na Kanembwa JKT iliyochezwaUwanja wa Kambarage ili kukusanya taarifa zaidi. Mechi hiyo haikumalizika.Bodi ya Ligi itakutana tena Jumapili (Novemba 17 mwaka huu).


FUTURE TAIFA STARS vs TAIFA STARS UWANJANI KARUME
Timu za Taifa za Future Taifa Stars na Taifa Stars zinacheza kesho (Novemba13 mwaka huu). Mechi hiyo ya kirafiki itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu yaKarume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.Mechi hiyo ni maalumu kwa Benchi la Ufundi la Taifa Stars linaloongozwa naKim Poulsen kuangalia wachezaji kumi kutoka Future Taifa Starswatakaoongezwa katika Taifa Stars tayari kwa mechi ya kirafiki ya kimataifaitakayochezwa Novemba 19 mwaka huu jijini Arusha.Watazamaji 300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh.5,000.



KUNDI LA NDEGE 3 LAJA NA MPYA TAMU YA MISUKOSUKO

KUNDI LA WANAMZIKI WAKONGWE LINALOUNDWA NA KHADIJA MNOGA (KIMOBITEL) , PAULYINE ZONGO NA JOAN MATOVOLWA WAKIMSHIRIKISHA GRAYSON SEMSEKWA  KATIKA WIMBO HUO MPYA UNAOITWA MISUKOSUKO

RAIS ATEMA PANDE LA DHAHABU, ATAKA LITUMIKE KULEA YATIMA!!!


THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS



Telephone: 255-22-2114512, 2116898 
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE, 
P.O. BOX 9120, 
DAR ES SALAAM.
Tanzania.




TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI


RaisKikwete arudisha zawadi ya dhahabu


Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameirudishia Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya MkoaniGeita zawadi ya gramu 227 za dhahabu safi akielekeza kuwa zawadi hiyoitumike kuwasaidia watoto yatima. 


Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu, Novemba 11, 2013, baadaya kukabidhiwa zawadi ya dhahabu hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua mgodi wa uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogo wa Kharuma ambako ndiko makao makuu ya wilaya mpya ya Nyang’hwale,Mkoa wa Geita.


Gramu hizo 227 ambazo ni sawa na aunzi nane zina thamani ya Sh. milioni 16 kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.


Baadaya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais Kikwete ameuliza: Sasa nifanye nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popote mnakotaka na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima.”


Akizungumzana wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete ameupongeza uongozi wamgodi huo akisema kuwa umeongeza thamani ya dhahabu na ya maisha yawananchi katika eneo hilo nje ya mji mdogo wa Kharuma.


Hatahivyo, Rais Kikwete ameushauri uongozi wa mgodi huo kufanya jitihada za kuboresha teknolojia inayotumika.“Mmefanya vizuri sana na mgodi huu ni mradi wa maana sana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili. Ubunifuhuu unastahili pongezi.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Lakini lazima tuboreshe teknolojia. Teknolojia inayotumika kwenye mgodi huu bado ni ya zamani kidogo. Hii ni sawa na hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii ya vipofu watupu. Yeye anaonekana kama mfalme.”


Mgodi wa Nyamigogo ambao ni mgodi wa marudio kwa maana ya kwamba unazalishadhahabu kutokana na mchanga ambao huko nyuma umepata kufuliwa nakutoa dhahabu, ulianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa zimewekezwa kiasicha Sh.bilioni 1.6 katika uendelezaji wa mgodi huo.

Risala ya uongozi wa mgodi huo inasema kuwa mgodi huo unaozalisha kiasi chagramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi na unaajiri watu 45 wakiwemo wanawake 10.


Tokea kuanzishwa kwake, mgodi huo umekuwa unaunga mkono shughuli za jamii inayouzunguka ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati na madarasa yashule katika vijiji viwili.


Rais Kikwete amezindua mgodi huo ikiwa sehemu ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika ziara yake rasmi ya kikazi katika Mkoa waGeita, moja ya mikoa minne ambayo aliianzisha mwaka jana. Mikoa mingine ni Simiyu, Njombe na Katavi.


Ziara hiyo ya siku tano inamalizika kesho, Jumanne, Novemba 12, 2013, na mbali ya kuzindua mgodi huo, Rais Kikwete leo amepokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Nyang’hwale na kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kharuma uliohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi. 


Imetolewana:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam.
11Novemba, 2013

Rais kikwete anatarajia kufanya majumuisho ya ziara yake Jioni ya leo!

Nov 5, 2013

SAFARI YA KICHAPO CHA M23 KATIKA PICHA

 HAPA ilikuwa Sept 15 ambapo mpaka baina  ya Kongo na Rwanda ulifungwa baada ya kutuhumiana  na hiii inafuatia Rwanda kudai Kongo imeua raia wake kwa kupiga kombora wakati ambapo kongo ilidai ni waaasi wa M23 walifanya hivyo kuongeza chumvi kwenye vita hiyo ili Rwanda aikasirikie kongo
 Hapa kikosi ch jeshi la Kongo kikisonga mbele baada ya kuanza kukomboa maeneo muhimu ya ngome ya waasi wa M23
 Baada ya mziki kuzidi jana usiku, M 23 Waliamua kuanza kuteketeza baadhi ya zana zilizokuwa zikiwasaidia, hii inaitwa bora wote tukose! hasa inapoonekana kuwa huna matumaini tena ya kwenda mbele zzaidi ya kutafuta mahala pa kujificha!!!
 Hii ndiyo iliyokuwa kambi ya M 23 Makao makuu yao, lakini baada ya kuvurumishwa wakaamua kuiteketeza kabisa jana na leo kabla ya kutangaza kisanii ati wameacha vita ili wafanye mazungumzo ya amani!
 Mateka na vijana waliojisalimisha kutoka kikundi cha M 23
 Zana zilizoharibiwa na kundi la M 23 baada ya maji kuwafika shingoni, hapa ni moja ya makambi yao katka eneo la Chanzo ambako ndiko makao makuu ya M23
 Upepo ulivyosoma vibaya waliamua kutelekeza mashine kama hizi za kivita na kutimua mbio kusikojulikana
 Kwaheri ya kuonana kifaa chetu, siye tunakwenda " ndivyo zana hii inavyoonekana kuachwa
 Hapa ndipo jamaa wa M23 walipojihifadhi kwa siku tatu za hivi karibuni lakini baada ya chai ya kuanzia jana jioni, usiku na hatimaye asubuhi ya leo wametangaza wenyewe kutupa chini mikoba
Hapa ni kambi yao iliyoharibiwa baada ya kukumbana na wakati mgumu wa jana na leo usiku!

Kiongozi wao amekuja na maelezo haya kwa kifaransa nitayafafanua


nnonce de fin de rébellion
Annonce de fin de rébellion

La Direction du Mouvement du 23 Mars annonce à l'opinion nationale et internationale qu'elle a décidé à dater de ce jour de mettre un terme à sa rébellion et de poursuivre, par des moyens purement politiques, la recherche des solutions aux causes profondes qui ont présidé à sa création.

A cet effet, le Chef d'Etat-major Général ainsi que tous les commandants des grandes unités de l'Armée Révolutionnaire Congolaise sont priés de préparer les hommes des troupes au processus de désarmement, démobilisation et réinsertion sociale dont les modalités sont à convenir avec le Gouvernement de la République Démocratique du Congo.

Fait à Kampala, le 05 Novembre 2013

Le Président du Mouvement du 23 Mars

Bertrand BISIMWA

Kwa kiswahili cha haraka haraka ni kwamba 


Mwisho wa Uasi
Mwisho wa Uasi
Kurugenzi ya  Movement on March 23 ama kwa kifupi M23 inalitangazia taifa na jumuiya ya kimataifa kuwa kuanzia tarehe ya siku ya leo kusitisha uasi wake, na sasa mazungumzo ya kisiasa yatachukua nafasi katika kutafuta suluhu  na kutafuta chanzo kilichotuleteleza kwenye hali hii ya mapigano

Kwa mwisho huu Amiri jeshi Mkuu na wakuu wa kamandi zake na vikosi  vyake (m23) wanatakiwa kuvunja vikosi  vyote, kuweka siraha chini  na kusitisha mapigano tena  ili kuunganisha nguvu na jamii ya watu wa kongo  wakati huu tuweze kutekeleza yale tuliyokubaliana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo


Limetolewa hapa Kampala ,November 5, 2013

Rais wa Movement of March 23

Bertrand Bisimwa

MCHANGO WA FM RADIO KUJENGA UELEWA KWA WANANCHI UKOJE?

Huyu ni mmoja wa watangazaji katika vituo vya FM akikuletea matangazo ya moja kwa moja kutoka uwanja wa Mashujaa Mkoani Njombe, anaitwa Hamis Kassapa akiripotia  UPLANDS FM ya Njombe. Yapo mambo mengi ya mafanikio yanayoweza kuelezewa na wananchi kama mafanikio ya uwepo wa vituo vya redio za FM kwenye maeneo yao ya karibu na hasa katika upashaji na utoaji elimu, je wewe unadhani ni jambo gani jipya ulilojifunza kupitia matangazo ya miongoni mwa vituo hivi?

Nov 4, 2013

MSIMU UMEANZA WA KILIMO, JE NA MWAKA HUU WANANCHI WATAUZIWA MBOLEA MBOVU?

 MWAKA ULIOPITA WILAYA YA MBOZI ILIKUMBANA NA MATUKIO YA UDANGANYIFU KWA MAKAMPUNI KUUZA MBOLEA ISIYOFAA KWA SHUGHULI ZA KILIMO
 HAPA IKIWA INAPAKIZWA KUREJESHWA DAR ES SALAAM KWAAJILI YA KWENDA KUHARIBIWA
GARI LINALOSAFIRISHA LIKIWA LIMEPIGWA KUFULI NA FUNGUO KUKABIDHIWA KWA ASKARI POLISI WALIOPEWA JUKUMU LA KUSINDIKIZA MBOLEA HIYO HADI DAR E SSALAAM

Na Mwandishi wa Indaba blog.
Msimu umeanza huku wananchi wakikumbuka vidonda vya msimu uliopita baada ya wafanyabisahara na makampuni kuwaingiza kingi kwa kuwauzia pembejeo zilizo na viwango vya chini ama zilizopitwa na wakati.

Itakumbukwa na wananchi wa wilaya ya Mbozi kuwa Mamlaka inayosimamia ubora wa Mbolea iliingia wilayani humo na kufungia moja ya maghala yanayouza mbolea hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa mbolea iliyoganda, lakini kwa mshangao wa wananchi baada ya miezi miwili kibali cha yule yule aliyefunga ghala hilo kilitolewa kikiagiza uongozi wa wilaya uruhusu ghala hilo liendelee na biashara.

Ni mazingira hayo hayo yanayowafanya wananchi kuwa na mashaka na msimu huu huku wakijiuliza je mambo yatakuwa yale yale kama ya mwaka jana?

Ni msimu huo wa mwaka jana ambapo wakulima waliuziwa mbegu za Mahindi zilizowekwa rangi ya mikeka kwenye viwanda vidogo vidogo vilivyopo mafichoni katika mji wa Mlowo ambapo licha ya makampuni yanayouza mbegu za mahindi kuitwa na kutoa ushahidi wakati wa ukamataji, ushirikiano ulikuwa mdogo hii ikidhaniwa kuwepo mikono ya wafanyakazi wa makampuni ya mbegu kwenye biashara hiyo haramu.

Ni msimu huo huo ambapo pia dawa za kupulizia mashambani zilipobainika kuuzwa zikiwa zimekwisha muda wake na hivyo kuendeleza wimbi na malalamiko kuwa shughuli ya Kilimo ni eneo la kutengeneza fedha za haraka haraka kupitia wakulima na hasa wakati wa msimu wa kilimo unapoanza ambapo kila kitu kuanzia zana za kulimia zinakuwa feki, mbolea feki, mbegu feki, madawa mengine feki na hadi vibarua feki!

Wakati hayo yakitokea, wataalamu wa Kilimo wilayani wanapasha kuwa kwa msimu huu mbolea inayotarajiwa kupatikana kwa wingi wilayani Mbozi ni Minjingu. majanga mengine haya!

Kwa muda mrefu kumekuwepo malalamiko kutoka kwa wakulima wakizungumzia kutofanya vizuri kwa mbolea hiyo wilayani Mbozi, lakini serikali kutokana na uzalendo kwenye makampuni ya ndani inasisitiza kuwa mbolea hiyo inafaa baada ya kufanya kitu kinaitwa "soil testing"

Licha ya hoja za wawakilishi wa wakulima kwenye vikao mbalimbali kutaka kujua mstakabali wa matumizi ya mbolea  hiyo ni wazi Minjingu imepewa heshima rasmi kutamba katika kilimo cha mahindi wilayani mbozi kwa lengo la kurejesha hali ya udongo ambao umeendelea kupoteza rutuba ya asili  kutokana na matumizi ya mbolea za kisasa za chumvi.

Nia ni njema lakini wakulima wanajiuliza majaribio haya yanafanyikia kwenye mikono yao wakati hali ya uhakika wa chakula haiashirii mbolea hiyo kuleta mafanikio? 

Nami najiandaa kwenda shambani nikitarajia kuwa serikali itakuwa sikivu pale nitakapouza debe moja la mahindi kwa bei ya kuruka kutokana na hatua zote za uzalishaji kuandamwa na ufeki hadi kunisukuma niuze kwa bei feki!!! kwaherini!!!

REFA ANAPOVUTWA MKONO ASITOE KADI KWA MCHEZAJI

HII ILIKUWA MCHEZO KATI  YA POLISI BUNDA NA KIMONDO YA MBOZI, MWAMUZI ALISHIKWA MKONO NA KUSHUSHWA WAKATI AKINYOSHA KADI YA NJANO KWA MOJA YA MCHEZAJI WA POLISI BUNDA

PALE UNAPOSHINDWA KUMWELEWESHA MTU, CHORA ARDHINI ATAELEWA TU


 Wakati mwingine kama haelewi, tumia michoro na alama ataelewa tu!

TAKWIMU MPYA ZA UKIMWI ZATOA AHUENI KIDOGO KWA MKOA WA MBEYA

 Mratibu wa Ukimwi Wilaya ya Mbozi akitoa somo kwa walimu walioajiriwa hivi karibuni  juu ya kutekeleza mpango wa mapambano dhidi ya UKIMWI mahala pa kazi
 Walimu wapya wakiwa katika majadiliano ya  makundi kuweka mikakati ya kushughulikia kwenye maeneo yao mapya ya kazi

Mmoja wa washiriki akiwasilisha mbele ya wenzake vikwazo vinavyochangia maambukizi na hatua zinazopendekezwa katika maeneo yao ya kazi

PAMOJA NA KUELEZWA SUALA LA MKOA MPYA LIMEKWISHA, WANANCHI WAHOJI NANI AMESIKILIZWA?

Wananchi wa eneo jipya linalopendekezwa kuwa Mkoa wa  Songwe wameendelea kuhoji mwelekeo wa suala hilo kutokana na awali kuleta mvutano kwenye vikao vya maamuzi na uongozi wa mkoa  kusukuma ajenda ya makao makuu isipewe uwanja wa kujadiliwa na baadaye kamati ya ulinzi na usalama ilibariki maamuzi hayo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema mapendekezo yanayoelezwa kusogezwa kwa mheshimiwa raisi ndiyo yale yanayopingana na mapendekezo ya wilaya zinazounda mkoa huo mpya ambapo suala la Makao makuu ya Mkoa huo mpya linalezwa kufanywa kwa kuridhishana 

Unajua kilichotokea ilifika mahala mwenyekiti akatamka " ninyi si mmepata jina la Mkoa, basi na wenzenu wapate makao makuu " alieleza mmoja wa wajumbe wakati akirejea yaliyojitokeza kwenye mchakato waugawanji mkoa kwenye vikao vya RCC

suala hilo lilichokonolewa kwenye kikao cha RCC hivi karibuni lakini, lilizimwa na Mwenyekiti kwa kueleza kuwa walishapeleka kwa Mh Rais mapendekezo na muhtasari wa maamuzi ya mkoa huo  na kinachosubiriwa sasa ni maamuzi ya Mh Rais kutangaza anavyoona yeye.

Licha ya wilaya za Mbozi,Ileje na Momba kufikia hatua ya kuhoji nani mwenye haki ya kufanya maamuzi ya maeneo yanayolengwa , Suala la kurejewa maamuzi ya makao makuu ya mkoa huo yameonekana kuwa na kigingi kizito kana kwamba hakuna utaratibu wa kujisahihisha kwenye utendaji wa serikali" anaeleza Mwananchi mwingine katika kujadili suala hilo

Suala hilo kwa sasa limeachwa mikononi mwa chama cha Mapinduzi katika kuliwasilisha kwa Mheshimiwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ili kuliangalia kwa mtazamo tofauti na ule wa watendaji wa serikali ambao wamewasilisha mapendekezo yanayolalamikiwa na wajumbe wa kikao cha RCC kutoka wilaya za Mbozi, Ileje na Momba kuwa msimamo wa mwenyekiti ulikuwa umejielekeza kupeleka makao makuu Mkwajuni.

Kwa taratibu za ziara za Mh Rais mikoani, pamoja na kupokea taarifa ya serikali kupitia mkuu wa mkoa, pia chama tawala huandaa tarifa yake na kuiwasilisha kwake ambapo huelezea kwa undani matatizo, changamoto na mafanikio ya ukuaji wa chama na utoaji huduma ambapo pia humulika kasoro za kiutendaji kwenye mkoa husika.
Inadhamiliwa kuwa suala la ugawaji mkoa wa Mbeya litajitokeza kwenye taarifa za chama sasa na hata
 katika ziara za mheshimiwa raisi atakazozifanya katika wilaya zinazounda mkoa mpya, na kuna wakati ambapo viongozi wa makundi ya jamii kama madiwani  kwenye vikao vyao wamewahi tamka kutaka kuendelea na mkoa wa zamani ili kuepuka mgawanyo wa mkoa usio na tija na hasa inapokuwa kwenye makao makuu yake.

Wengi wanatafsiri hali hiyo kuwa ina msukumo wa aliye na kisu kikali ndiye hula nyama, kwa maana ya kuwa Naibu waziri wa elimu Mh Mlugo amekuwa na "influence" katika kufikia maamuzi ya kupeleka makao makuu ya mkoa wa Songwe kwenye eneo lake la utawala (jimboni mwake) kwa kufanya ushawishi kwenye meza ya mwenyekiti wa RCC.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh Abas Kandoro alishatoa ufafanuzi mara kadhaa juu ya kuhusishwa na kupindisha maamuzi ya ugawaji wa mkoa na hususani suala la makao makuu yaliyopendekezwa kuwa Mkwajuni, kuwa suala hilo limezingatia vigezo na nimaamuzi yaliyobarikiwa na kamati ya ulinzi na usalama.

Alishafafanua kuwa hana maslahi yoyote na maamuzi hayo kwakuwa yeye si mkazi wa mkoa wa mbeya na kwamba akishastaafu atarejea mkoani kwake Iringa, hivyo msukumo wa kupeleka makao makuu wilayani Chunya ni katika kuhakikisha dhana ya maendeleo kwa uwiano inazongatiwa.

Suala hili sasa  limebakia likijadiliwa kwenye makundi ya Kisiasa na hasa kwenye chama cha Mapinduzi ambapo mijadala ya kusimamia misimamo na maslahi inaonekana kuchukua nafasi zaidi, huku vigezo vya maamuzi vikionekana kutowekwa mezani mapema kabla mchakato huo haujaagizwa kuanza kwenye ngazi za chini.


MITIHANI YAANZA KWA UTULIVU

Add caption
WASIMAMIZI WA MITIHANI WAKIFANYA MAANDALIZI YAO YA MWISHO JANA ASUBUHI KWAAJILI YA KUFIKISHA MITIHANI KATIKA MENEO YAO

INDABA AFRICA NA UONGOZI WAKE TUNAWATAKIA MITIHANI YENYE MAFANIKIO WAHITIMU TARAJIWA WA MWAKA 2013 NA UFAULU MZURI

Nov 3, 2013

WAZAZI WAPONGEZA NECTA KUWAHI NA KUTOA MATOKEO SAHIHI

Baada ya NECTA kutoa matokeo ya darasa la saba haraka na kwakupitia wavuti yao, wazazi wamepokea matokeo hayo kwa mtazamo chanya huku wakisifu maboresho yaliyofanywa na NECTA
Kwa nyakati tofauti wazazi wanasema, NECTA imeondosha malalamiko ya muda mrefu juu ya mfumo wa usahihishaji ambao ulikuwa unalalamikiwa hasa kwa watu wenye mwandiko usio mzuri

Wanasema kupitia usahihishaji wa sasa Optical Mark Leader, unaonyesha kuwa  umeleta ufanisi na kuwahi kutoa matokeo kwa muda mfupi.
 

Nov 2, 2013

MATOKEO DARASA LA SABA KITAIFA, SHULE YA ASIYESOMA YAONGOZA MKOA WA MBEYA



NA INDABA AFRICA

Shule ya mfanyabiashara  maarufu wilayani Mbozi Bwana Lington Chaula ambaye hakufanikiwa kupata elimu miaka yake ya ujana, imeshika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Mbeya na nafasi ya tisini kitaifa katika matokeo ya darasa la saba yaliyowekwa hewani jioni hii

Ilasi imekuwa shule ya  kwanza kimkoa na pia ya kwanza katika wilaya ya Mbozi kwa kuwa na wanafunzi 29 ambapo kati yao waliopata wastani wa daraja la  A (kwanza) ni  11 na waliobakia wamepata daraja B.

Matokeo hayo yanaonyesha pia shule mojawapo isiyotarajiwa ya IZYANICHE iliyopo kwenye moja ya pori la wilaya Mbozi imefanya vizuri kwiwilaya na kuchukua nafasi ya tano

Kwa matokeo hayo, inathibitisha nia ya Mzee Chaula kuonyesha kusikitishwa kwake kwa kushindwa kupata elimu bora na kudhamilia kuwapa fulsa watanzania wengine kupitia uwekezaji alioufanya kwenye elimu kuanzia chekechea hadi kidato cha sita.

Mzee Chaula katika moja ya vipindi vilivyorushwa na TBC mwanzoni mwa mwaka huu alikaririwa akifafanua mbele ya mwandishi aliyekuwa akimhoji kuwa anajisikia uchungu anapoona watoto hawapati elimu na kuendelea kuzurura mitaani

Katika hali ya kuonyesha kujali suala la elimu alifika mahala akatoa machozi wakati akizungumzia adha ya kutokuwa na elimu huku akikumbuka namna ambavyo kwa upande wake alikosa elimu.

Alisema wakati akiwa tayari amejiimarisha kibiashara alilazimika kuajiri mwalimu wa kumfundisha kiwango ambacho kilimwezesha kumudu majukumu ya biashara zake na kwenda na teknolojia za sasa ikiwemo matumizi ya kompyuta kwaajili ya kutunza kumbukumbu mbalimbali za biashara zake.

Anasema ni mazingira hayo yalimsukuma kuanzisha shule kama moja ya maeneo ya uwekezaji ambapo alianzisha Ilasi English Medium School ambayo iliwezesha pia kuanzishwa kwa shule za sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne, na tano hadi sita.

Kwa sasa kampuni ya Ilasi pia inamiliki kituo cha Redio cha Ilasi FM ambacho kimeendelea kuwa zana muhimu ya kutoa elimu katika jamii na kuongeza kasi ya mabadiliko ya fikra miongoni mwa wananchi katika maeneo kinakosikika mkoani mbeya pamoja na mikoa jirani.

Shule maarufu mkoani mbeya za Umoja, St. Mary's, Mkapa na zingine nyingi zimefungashwa tela na Ilasi iliyopo wilayani Mbozi kwa matokeo hayo ya darasa la saba.

Kwa matokeo haya, sekeseke la walimu wakuu kujichuja kutokana na shule zao kufanya vibaya ndiyo msimu wake ambapo inatarajiwa kuwa katika vikao vya madiwani, yataibuka ya kwanini shule fulani imetuwakilisha vibaya?