Adverts

Jan 26, 2014

DALILI ZA MKOA WA SONGWE KUTANGAZWA ZIPO KARIBU IMEFAHAMIKA


MKOA MPYA WA SONGWE UNAOPENDEKEZWA NA WILAYA TATU ZA MBOZI, MOMBA NA ILEJE AMBAO KUNA KILA DALILI KUELEKEA KUIVA LICHA YA VIKWAZO NA CHANGAMOTO ZA HAPA NA PALE- HAYA YALIKUWA MAPENDEKEZO YA AWALI YA WILAYA YA MBOZI KWENYE ANDIKO LAKE LILILOPITISHWA NA DCC AMBAPO ENEO LAMKWAJUNI LILIPENDEKEZWA KUUNDWA WILAYA MPYA YA MKWAJUNI - MAPENDEKEZO HAYO YANAOKENA KUKUBALIWA KWENYE HATUA ZA MAJADILIANO AMBAPO WAZIRI MKUU  HIVI KARIBUNI ALIMTUMA WAZIRI WA TAMISEMI HAWA GHASIA KUTEMBELEA MKOA WA MBEYA NA KUONA UWEZEKANO WA KUSHAURI KUANZISHA MCHAKATO WA UKATAJI WA WILAYA YA CHUNYA ILI KUPATA WILAYA MPYA YA MKWAJUNI MCHAKATO AMBAO UMEANZA!.
KWA HATUA HIYO NI DHAHIRI MKOA WA SONGWE MAKAO MAKUU YAKE YATAKUWA WILAYA YA MBOZI HIVYO WILAYA YA MKWAJUNI KUWA SEHEMU YA WILAYA ZITAKAZOUNDA MKOA WA SONGWE 
HIVI NDIVYO MAPENDEKEZO YA KUUGAWA MKOA WA MBEYA YALIVYOANZA NA MIPAKA YA MKOA MPYA NA ULE WA ZAMANI NDIVYO INAVYOONEKANA IKIHUSISHA PIA WILAYA MPYA INAYOPENDEKEZWA YA MKWAJUNI!. IKIWA MHESHIMIWA RAISI ATATOA BARAKA ZA KUUTANGAZA MKOA WASONGWE KWENYE MAADHIMISHO YA  MIAKA 37 YA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOANI MBEYA  NA KUTOA UTATA WA MAKAO MAKUU YA MKOA HUO, NI DHAHIRI ITAKUWA ZAWADI YA MWAKA 2014-2015 KWA WANANCHI WA MIKOA HIYO NA HASA MKOA MPYA UNAOUNDWA NA WATU WAPATAO MILION 1.2