Adverts

Jan 22, 2014

KWAHERI CHILEWA KWENYE UTUMISHI WA UMMA- MBOZI WASEMA UMETIMIZA ENEO LAKO!

 Aliyekuwa mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Bw Levison Chilewa akishuka rasmi kwenye gari la ofisini kwake wakati wa sherehe za kumuaga baada ya kustaafu kwenye utumishi wa umma na kuwa raia mwema
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mbozi  Daktari Charles Mkombachepa kwenye hafla ya kumuaga bwana Chilewa
 Mshereheshaji bwana Msokwa akianzisha shughuli hiyo katika ukumbi wa Cathoric Centre Mkonongo

 Mkuu wa mkoa wakichart chambo na Bwana Chilewa kushoto kwa mkuu wa mkoa ni mkuu wa wilaya ya Mbozi Dk. Kadeghe
 Kaimu Mkurugenzi Daktari  Charles Mkombachepa akitoa neno kabla ya mambo kuchanganya kwenye sherehe hiyo
 Waheshimiwa madiwani wakipunga mkono wa kwaheri kwa aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuiwezesha mbozi kupandisha mapato yake ya ndani kutoka milion 400 alifohamia mwaka 2006 hadi kufikia Bilion 3 anapoondoka

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Minga akizungumza jambo kwenye hafla hiyo ambapo alieza kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kukumbuka alama za maendeleo zilizoasisiwa na Bwana Chilewa ikiwemo miradi inayoendelea kutoa huduma kwa wananchi wake zikiwemo kituo cha mabasi cha Vwawa, Uanzishaji wa mamlaka ya mji wa Tunduma, mgawanyo wa wilaya ya Mbozi na kupata wilaya ya Momba  na uimarishaji wa huduma za jamii hasa miundombinu, barabara , mawasiliano na michezo pia

 Kitu kilijibu! hapa Hamisi Mtoni Majani mratibu wa TASAF Mbozi na Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Wakili msomi Deogratius Nchimbi wakizibua shampeni
 Wakuu wa idara wakipanda kwa kwaito wakiongozwa na Kitashu the great" meneja mamlaka ya maji mji wa Vwawa

 Watumishi wa idara ya afya nao wakatoka na jamii ya ndombolo !!
 Kamati ya Ulinzi na Usalama wakaingia na staili ya kunyemelea !!!
 Mtendaji wa Mtandao wa Indaba africa alikuwemo pia
 Kaimu katibu Tawala Mkoa Bwana Magacha alikumbushia maisha yake ya Mbozi na hatimaye ushirikiano alioupata hadi alipoteuliwa kuwa Afisa Tawala Mkoani
 Ilikuwa ni furaha kwa Bwana na Bibi  Chilewa  baada ya kubaini watu wamejitokeza wengi kumuaga ikiwa ni dalili ya maisha aliyoishi na wakazi wa wilaya ya Mbozi yalikubalika
 Mwenyekiti akaanzisha kusakata lumba
 Timu ya madiwani ikielekea kumpa mkono wa kwaheri bwana Chilewa
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Erick Minga akipeana mikono na bwana Chilewa ya kwaheri
 Bwana Rashid Mbegu Moja ambaye alikuwa District Treasury akiagana na mama Chilewa, hata yeye pia baada ya siku chache akapata uhamisho
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Kandoro akitoa salam zake
shughuli ilimalizika kwa Msosi