Mmoja wa makada wa CCM wilayani Mbozi Bwana Ndisana akikumbatiana na Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mh Godfrey Zambi baada ya kupokelewa katika mpaka wa Mbeya na Mbozi leo mchana
Wakazi wa Vwawa na vitongoji vyake waliojitokeza kumpokea mbunge wao baada ya kuteuiliwa kuwa naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
WanaCCM nao hawakuficha sura kwenye shughuli hii walijipambanua kwa chama chao kuwakilishwa na mwenyekiti wa mkoa wa mbeya kwenye uongozi wa wizara muhimu inayogusa maisha ya watanzania kila siku
Mh Zambi akiwasili eneo la mapokezi mpakani mwa wilaya ya Mbozi na Mbeya
Wadau mbalimbali walikuwepo kwenye tukio hilo la mapokezi
Madiwani pia walikuwa miongoni mwa walioshiriki kwenye mapokezi hayo, hapa ni bwana Kasebele akikumbatiana na mbunge wake
Katibu Tarafa ya Vwawa Bi Kasunga akisalimiana na Mh Zambi
Afisa Mipango halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Ngoi Elisey akisalimiana na naibu waziri mara baada ya kupokelewa katika viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Mbozi na kusomewa taarifa ya maendeleo ya wilaya
Hapa mheshimiwa Zambi akiwa na Mbunge wa Nkasi jukwaani
Zambi akimtambulisha mkewe kwenye mkutano ulioandaliwa na chama cha mapinduzi nje ya ofisi za chama za wilaya ya Mbozi
Na Danny Tweve Mbozi
Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika amewatoa hofu watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi kuwa hana mpango wa kuwashushia makombora na kuwaandama baada ya kuteuliwa nafasi ya Naibu waziri wa kilimo, chakula na ushirika
Akizungumza wakati akipokea taarifa ya wilaya ya Mbozi katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mbozi, Bwana Zambi amesema, amepokea taarifa kuwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi wamejazwa hofu baada ya uteuzi wake na kwamba ana mpango wa kuwang'oa na kuwashughulikia baadhi ya watumishi
"nimesikia kuwa eti nina orodha ya watumishi ninaokusudia kuwashughulikia hapa halmashauri, naomba niwatoeni wasiwasi endeleeni kuchapa kazi, sitatumia madaraka yangu niliyopewa na raisi kuwaandama watumishi wa halmashauri hata kidogo" alieleza mheshimiwa zambi
Alisema hali hii ya kuwajaza hofu watumishi, pia imejitokeza kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wamekuwa wakishambulia uteuzi huo kuwa unatamsababishia Zambi asionekane jimboni, jambo ambalo amelifafanua kuwa, majukumu ya Naibu waziri yatamwezesha kuonana kwa karibu na wananchi kwakuwa wanapewa muda mara nne kwenye kipindi cha mwaka kurejea majimboni mwao