Wajumbe waliohudhulia kwenye chanzo cha maji katika eneo la Halungu ambako mradi mkubwa wa maji utajengwa
Mhandisi wa Maji Mbozi Eckson Mwasyange akizungumza kwenye uwekaji jiwe la msingi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Ambakisye akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Halungu
Chifu Mlotwa Shantiwa akipanda mti kwenye uzinduzi wa mradi wa maji Halungu
Wakuu wa idara na wakazi wa Halungu wakipanda miti katika chanzo cha maji Halungu
Mwandishi wa TBC Hosea Cheyo akiongozana na chifu Mlotwa Shantiwa
Diwani wa kata ya Halungu Mh Simkoko akizungumza na wakazi wa kijiji hicho juu ya mradi wa maji unaotarajiwa kutekelezwa
Wazee wa kinyakyusa wakiingia kwa mbwembwe kwenye Ling'oma
na Mwandishi wa Indaba Africa-Mbozi
Mwenyekiti wa baraza la machifu wilayani Mbozi katika mkoa wa
Mbeya Chifu Mlotwa Shantiwa ameitaka serikali kuachia baadhi ya mambo na hasa
masuala ya adhabu kwamakosa ya uhifadhi
wa mazingira kwa mamlaka za kimila ili kuwezesha kujenga nidhamu katika jamii.
Akizungumza katika kijiji cha Halungu wilayani Mbozi, chifu
huyo amesema sheria za kitaalam zimeonekana kushindwa kufanya kazi hasa kwenye
uhifadhi wa vyanzo vya maji ambapo hali imeendelea kuwa mbaya licha ya sheria
hizo kuwepo
Alisema ili kujenga nidhamu na kutia uoga katika jamii, ni
vyema machifu wakaachiwa sehemu ya majukumu ya kuadhibu wanaoharibu mazingira
ili kuwezesha vizazi vijavyo angalau kufaidi sehemu ya raslimali zilizopo
Aliyasema hayo wakati wa kuwekwa jiwe la msingi la mradi wa
maji kwa vijiji vya Halungu na Sasenga vyenye zaidi ya wakazi 9,500, mradi
ambao utagharimu jumla ya shilingi million 668 mpaka kukamilika kwake.
Mapema akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Ambakisye ameelezea kusikitishwa na ari ndogo ya
uchangiaji asilimia 5% ya mradi ambapo katika kipindi cha miaka minne wananchi
wamechangia shilingi million moja tu kati ya shilingi 32 milion walizopaswa
kuchangia.
Alisema hali hiyo inaweza kukwamisha uwezekano wa fulsa
zingine za miradi ya maendeleo kuelekezwa kwa wananchi hao.
Kulingana na mhandisi
wa maji wilaya ya Mbozi bwana Ackson Mwasyange, mradi huo utaanza kutekelezwa mwezi April na
unakusudiwa kukamilika mwezi March 2015, na kwamba ni miongoni mwa miradi
mingine mitano inayotekelezwa wilayani Mbozi kwa kupitia program ya maji chini
ya benki ya dunia.
Katika
risala yao wananchi wa kijiji hicho wameonyesha kusikitishwa na ucheleweshaji
wa mradi huo ambapo tangu mwaka 2004 serikali ilianzisha mchakato wa
utekelezaji wa miradi hiyo mpaka sasa bado zimeendelea kutolewa taarifa za
matumaini pasipo kupata huduma ya maji.
Mwisho