Sakata la ndege wa ajabu katika kisiwa cha Musira mkoani Kagera wanaotoa kinyesi kinachodaiwa kuwa na sumu na kusababisha kuku na mbuzi kuteketea sasa taarifa za kitaalum zimedai kuwa 7% ya watoto na 3% watu wazima wameathiriwa na kinyesi kutokana na kushindwa kupumua vyema.
Hayo ni sehemu ya matokeo ya dodoso la uchunguzi kuhusu ndege hao kwenye Manispaa ya Bukoba, ambapo afisa tarafa ABDON KHAWA ameitoa taarifa hiyo ya kitaalam mbele ya mkuu wa mkoa wa Kagera Fabian Masawe alipotembelea kisiwa hicho jana.
Bwana Kahawa amesema kuwa taarifa hiyo inaonesha asilimia 45% ya mapaa ya nyumba za mabati yamepata kutu na kutoboka kutokana na kinyesi cha ndege. Kulingana na taarifa hiyo asilimia 61% ya kuku na 6% ya mbuzi wamekufa kutokana na vinyesi.

Mh Diwani kata Miembeni Richard Gasper Asilimia ya wakaazi wa Musira wanaupele na kuwashwa ngozi baada ya uvamizi wa ndege. |