Adverts

Mar 19, 2014

TUNDUMA MADEREVA WAFUNGA BARABARA, KISA DEREVA WA TANZANIA KUUMIZWA NA POLISI ZAMBIA

HABARI ZILIZOTUFIKIA MUDA HUU , NI KWAMBA SHUGHULI ZA MPAKA WA TUNDUMA NA ZAMBIA ZIMESIMAMA KWA MUDA BAADA YA ASKARI WA UHAMIAJI UPANDE WA ZAMBIA KUMJERUHI VIBAYA DEREVA WA ROLI LA UPANDE WA TANZANIA.
 
TUKIO HILO LIMETOKEA MAJIRA YA SAA 5.30 ASUBUHI BAADA YA DEREVA HUYO AKIWA ANAKAMILISHA TARATIBU ZA UHAMIAJI UPANDE WA NAKONDE, KULITOKEA UBISHANI KUDOGO ULIOPELEKEA KULAZIMIKA KUTOKA NJE ILI AWASILIANE NA TAJIRI WAKE KWA SIMU
 
KATIKA HALI YA MVUTANO HUO, NDIPO DEREVA HUYO ALIPOVAMIWA NA POLISI WA UPANDE WA ZAMBIA BAADA YA KUAMRIWA NA OFISA WA UHAMIAJI WA UPANDE WA ZAMBIA KUMKAMATA KWA KUHOFIA ALIKUWA AKIRIPOTI MAHALA MALALAMIKO YA NAMNA ALIVYOTENDEWA NA OFISA HUYO
 
DEREVA ALIDAIWA KUHUSISHWA NA MGOGORO HUO ALIKUWA NA ROLI LENYE NAMBA ZA USAJIRI T 131 AQU MALI YA KAMPUNI YA CITEX YA JIJINI DAR ES SALAAM
 
KATIKA KUHOJI SABABU ZA KUZUIWA KUZUNGUMZA NA SIMU, NDIPO ALIPOANZA KUCHUKUA KICHAPO CHA KITAKO CHA BUNDUKI MAENEO NYETI.
 
KONDA WAKE ALIVYOSHUHUDIA HALI HIYO ALIWATAARIFU MADEREVA WENZAKE NA NDIPO WALIPOAMUA KUFUNGA NJIA KWA MAGARI HATUA AMBAYO IMESABABISHA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI MPAKANI KUSITISHWA
 
SAA SABA KAMILI KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA UPANDE WA TANZANIA ENEO LA MPAKANI IMEINGIA UPANDE WA ZAMBIA KWA LENGO LA KUJADILIANA HALI HIYO KUPITIA UTARATIBU WA UJIRANI MWEMA AMBAO HUHUSISHA MAMLAKA ZA ENEO HILO.