Kikosi cha ASHANTI kilichoshuka dimbani dhidi ya Kimondo na kuambulia kichapo cha 2 Oclock |
Hii ndiyo sumu ya Ashanti al maarufu kama Kimondo KISSC iliyoshuka jioni ya leo na kutoka na ushindi wa mabao matakatifu 2-0 |
Benchi la Kimondo
Na Danny Tweve wa Indaba Africa,
Ikicheza uwanja wake
wa nyumbani Kimondo SSC ya Mbozi imeendelea kutunisha msuri kwa timu za maji ya
chumvi , mara hii kwa kuibatua Ashanti United
mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi
daraja la kwanza uliofanyika uwanja wa CCM Vwawa.
Hadi mapumziko , si
Kimondo wala Ashanti walikuwa wamechungulia nyavu za timu pinzani licha ya
Kimondo kukosa mabao matatu ya wazi katika gonga zilizochezwa kwenye lango la
ASHANTI lakini papara za wachezaji wake ziliiharibu mabao hayo.
Kipindi cha pili
kilianza kwa mabadiliko ya mfulizo yaliyofanywa na kocha wa timu ya Ashanti
ambayo yaliongeza uhai na mashambuzi, gonga na viminyo vya hapa na pale, hata
hivyo michezo ya kimjini mjini –zikiwemo rafu za hapa na pale, vipepsi na janja
janja ziliwagharimu Ashanti kwa
wachezaji wake wawili kupewa kadi za njano kwa kuwajeruhi wachezaji wa kimondo
ambao mmoja alishindwa kuendelea na mchezo.
Mnamo dakika ya 72
Kimondo kupitia kwa Michael Mwailusu
Bosco baada ya kutokea gonga nikugonge langoni mwa ASHANTI
kufuatia kona iliyopigwa na Mshaki Simbeye
Dakika ya 89 Kimondo
walitupia msumari wa moto langoni mwa Ashanti ulioenda moja kwa moja wavuni
bila mlindamlango kuuona mpira ulioanzia wingi ya kushoto , bao lililofungwa na
Geofrey Mwashuya ambaye katika mchezo huo alionekana wazi kuwa hatakuwa na timu
ya Kimondo kwenye dirisha dogo la usajiri kutokana na kiwango chake kuendelea kuvutia timu nyingi
za ligi kuu.
Ama kwa upande wa
mashabiki, burudani ya mchezo wa leo iliongezewa chachandu baada ya mashabiki
wa Mbeya City kukodi mabasi mawili kuja
kuipa sapoti Kimondo ya Mbozi hali ambayo iliufanya uwanja ulindime kwa shamra
shamra na mbwebwe za mashabiki hao.
Mchezo wa leo
uliochezeshwa na mwamuzi Kinugani kutoka Morogoro akisaidiwa na Alphaxad Mteta
kutoka Ruvuma, Cheyo kutoka songea , Kefa kayombo kutoka mbeya ulikuwa chini ya
kamisaa Zahra Mohamed mwamuzi wa siku
nyingi wa michezo ya kimataifa.