Adverts

Oct 11, 2014

KIMONDO YAANZA KWA AMSHA AMSHA KAMA ZA MBEYA CITY, YAIBUTUA VILLA SQUARD 2 'OCLOCK!


Timu ya Kimondo katika mchezo wake na Villa Squard ikiwa kwenye ng'ari nga'ari mpya

Timu ya Villa Squard katika pozi lapicha kabla ya mchezo huo

Ng'ari ngari ya Kimondo ambao ndiyo uzi mpya utakaotumika katika kipindi chote cha ligi , mashabiki wake wameahidi kuendesha harambee ya kuichangia timu hiyo ili kuiwezesha kuanzisha mradi wa TSHIRTS ambao utaingiza mapato kwa timu

KIMONDO SUPER SPORTS CLUB ya Mbozi imeanza vyema ligi daraja la kwanza kwa msimu wa pili tangu ipande daraja, kwa kuwainua mashabiki walifurika uwanja wa CCM Vwawa baada ya kuwanyunyizia mabao 2 kwa 0 timu ya Villa Squard ya jijini Dar

Ikiingia na Ng'aring'ari kali zinazoinyemelea Mbeya City, pamba kali za blue bahari moja makini sana, ilianza kuonyesha mazingira ya ushindi tangu dakika za mwanzo kutokana na mashambulizi ya mfululizo kuanzia dakika ya 35 hadi  kipindi cha mapumziko ikiwa na bao moja mkononi
Bao la Kwanza kwa Kimondo lilipatikana mnamo dakika ya 41 kupitia kwa Geofrey Mlawa baada ya kazi nzuri iliyofanywa na  Geofrey Mwashuya ambaye alikuwa lulu kwa kuendesha mchakamchaka beki ya Villa muda wote

Dakika 45 za kipindi cha pili zilianza kwa kosa kosa nyingi zilizoiandama Kimondo baada ya kufanya mabadiliko kwa kumpumzisha Gofrey Mlawa ambaye alijeruhiwa dakika chache kabla ya mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Dulla Jumanne, ambaye aling'ara kwa kuamsha mashambulizi ya mfululizo yaliyoipeleka Kimondo hatua ya kupata penati
Ilikuwa dakika ya 83 Geofrey Mwashuya aliihadaa ngome ya Villa kwa shuti lililomfikia Peter Methew ambaye akaunga msafara wa kwenda kumwona Kipa wa Villa Squard lakini kabla hajafanya mambo alivutwa jezi na mzee mzima Nurdin Bakari na hivyo mwamuzi kutoa penati kwa Kimondo ambayo ilifungwa na Mpoki Tauson ambaye aliihesabia Kimondo bao la pili dakika ya 85.

Baada ya bao hilo Villa waliamua kutembeza viatu mwanzo mwisho hali ambayo ilimfanya mwamuzi Salehe Mang'ola kutoka Dodoma kumzawadia kadi ya Njano Ramadhan Chombo Lidondo na mara kadhaa kujizuia kutoa kadi kutokana na makosa ya wazi wazi .
Dakika ya 88 Villa walifanya shambulio lililojengwa na mzee mzima Nurdin Bakari na kusababisha mmoja wa wacheza wa Kimondo kuunawa eneo la hatari na kusababisha penati ambayo hata hivyo mashabiki wa Villa wakiwa na matumaini ya kupoza mioyo kwa bao angalau 1, Mchezaji wao aliyevaa jezi 25 alipiga penati hiyo nje na kuufanya mchezo kumalizika Kimondo 2 Villa Squard 0