Adverts

Sep 27, 2010

KIJIJI KIMEZUNGUKWA NA UTAJIRI LAKINI CHENYEWE MASKINI

Wakati wawekezaji wa maru maru wakiendelea kufaidi matunda ya uhuru, upande wa pili hiki ndicho kijiji kilichopo kando ya mradi huo ambacho wananchi wake wanategemea kudra za mwenyezi mungu katika kuendesha maisha yao, baya kuliko yote ni kwamba hakuna msaada wowote ambao umetolewa na wadau hao wa maendeleo kusaidia hata miundombinu ya kuunganisha wananchi hawa na barabara kuu ya Songwe Mbozi ambayo inapita umbali wa km3 kutoka eneo la mradi, cha mno zaidi hata shule ya msingi imekaa kama vile hakuna wawekezaji kwenye eneo hilo. Mungu isaidie Mbozi.

SHIMO LINALOTOKEZA ZIWA RUKWA

Shimo lenye urefu wa zaidi ya kilometa 300 linalotokeza kwenye mwambao wa ziwa Rukwa likionekana baada ya mdau wa blog kuingia kwa umbali wa mita 200 na kupata picha vertically!!! karibuni kwa utalii mbozi.

HUU NDIYO MWAMBA WA KALE

Sehemu ya mwamba mkubwa wa jiwe linalochongwa na kutengenezwa maru maru liliwa bado linasubuli wawekezaji waendelee kulitafuna" kwa ujumla utajiri huu ulitakiwa kuibadili hali ya wilaya ya Mbozi na fikra za wananchi wake kutoka kwenye kufikiri kijima kama matukio ya uhalifu,ujambazi na mauaji ya uchunaji ngozi na hatimaye ikawa nchi ya ahadi na maendeleo ya kiwango cha juu ikiwa raslimali kama hizi zingetumika kwa mrahaba mnono kurejeshwa kwa wananchi badala ya wawekezaji kuingia na kuharibu mazingira na kuacha maelezo kuwa wizara ndiyo inajua yote!

MARU MARU INAPATIKANA MBOZI

Hii ni sehemu ya utajiri wa Mbozi ambao kampuni moja ya kigeni imekuwa ikinufaika na raslimali hii pasipo kuilipa halmashauri ya wilaya chochote kwa maelezo kuwa vibali vimetoka wizrani(wizara inayoshughulikia masuala ya nishati na madini). Hii kitu ni mawe yaliyochongwa kwaaajili ya kwenda kukatwa vipande vidogo vidogo kama maru maru kwaajili ya nakshi ya nyumbani. Kigae kimoja cha ukubwa wa cm 30 huuzwa kati ya shilingi 50,000 hadi 70,000. piga mwenyewe hesabu kwa jiwe kama hilo moja bei yake vipi?????kalagabahooo!!

Pango la Popo wilayani Mbozi

Hili ndilo pango la Popo lilipo eneo la Songwe wilayani Mbozi, eneo hili lina akiba kubwa ya mbolea ya Popo ambayo imeonyesha mafanikio makubwa katika kilimo cha mboga mboga, bustani za maua nk. Inakadiriwa kuwa shimo hilo lina zaidi ya popo Milion 5 na kiwango hiki kimeshuka kutokana na wakazi wa vijiji vilivyo karibu na pori lenye pango hilo kuamua kufakamia ndege hao na kuwala (kitoweo).

WAWEKEZAJI WANAPOJICHOTEA

Hii ndiyo raslimali ya udongo unaotumiwa na kiwanda cha saruji Mbeya kwaajilio ya kutengeneza Saruji aina ya Pozolana ambayo ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini, nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda. Udongo huu unapatikana katika kijiji cha Ivugula hata hivyo bado haijawa wazi wananchi wa maeneo haya na halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa ujumla inanufaikaje na mradi huu kwakuwa Kiwanda kwa upande wake inaendelea kunufaika na uuzaji wa saruji lakini wananchi wenyewe hoiii

MDAU WA BLOG AKIWA KWENYE KAZIII

Ni katika mazingira ya kuandaa Documentary ya vivutio vya asili vilivyopo wilayani Mbozi . Hapa ni Bonde la Mto Songwe eneo ambalo lina vivutio lukuki vikiwemo, maji moto yanayotokana na volcano, shimo linaloenda urefu wa zaidi ya kilometa 300 hadi kwenye ziwa rukwa, pango la popo, pango lililokuwa likitumiwa na machifu kujificha wakati wa vita za makabila

Sep 26, 2010

WANAHABARI WATAHADHARISHWA KULINDA MAISHA YAO

Wandishi wa habari wametahadharishwa kuwa wasijiweke katika mazingira ambayo yatawafanya wapoteze maisha kwa dhana kuwa wanaripoti ukweli hasa nyakati hizi za uchaguzi kwa kuzingatia kuwa bado vyombo vingi vya habari havijatengeneza mazingira ya kulinda maisha ya wanahabari na familia zao. Akizungumza katika mafunzo ya siku moja ya kupitia Maadili ya uandishi wa habari za uchaguzi 2010, afisa habari kutoka shirika la umoja wa mataifa la maendeleo-UNDP bwana Sebastian Sanga amesema wandishi wa habari wanapaswa kujali maisha yao zaidi kuliko kujiweka mbele wakati hawana bima za maisha yao. alisema kazi ya uandishi wa habari haitakuwa bora ikiwa mwandishi atajihatarishia maisha yake kwa kujiweka mbelembele wakati ambapo mazingira wanamofanyia kazi hakuruhusu hali hiyo. alihoji kama kuna mwanahabari miongoni mwa wandishi 50 waliohudhulia mafunzo hayo kama yupo aliyekatiwa bima na chombo chake cha habari anachoandikia. hata hivyo ilibainika kuwa wengi wa wandishi hao hawana bima na akaendelea kuwaeleza kuwa maisha ni bora kuliko kitu chochote kile na kwamba si lazima mtu akapoteza maisha yake eti kwakuwa anakitumikia chombo chake cha habari kwa kufanya uchokonozi wakati ambapo chombo anachokiandikia hakijaweka mazingira mazuri kwake ya kufanya kazi hizo. Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kujali zaidi maisha na uhai wa mwandishi binafsi badala ya kujiweka mbele kujali maslahi ya chombo unachoandikia kwakuwa miongoni mwa wanahabari wenyewe wamekuwa wakiuzana. Wakati akizungumzia hali hiyo wengi wa wanahabari walionekana kupoteza pumzi hasa kwa kukumbuka mazingira wanayofanyia kazi kuonekana kuwa ya manyanyaso makubwa kutoka kwa vyombo wanavyovitumikia ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kupima habari zao kwa kutumia rula ili walipwe.

UCHAGUZI MKUU RIDHIWAN KIKWETE ATIA TIMU MBOZI

Mtoto wa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi RIDHIWAN KIKWETE jana alipokelewa kwa mbwembwe na wanachama wa chama cha mapinduzi Mbozi akitokea wilayani Ileje. Ridhiwan ambaye ni Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya umoja wa vijana Taifa pia akiwa mwenyekiti wa Miradi ya umoja wa Vijana wa CCM aliwasili katika ofisi za chama za wilaya Mbozi majira ya saa 11.20 Jioni. Inaelezwa kuwa pamoja na kuzungumzia masuala mbalimbali ya kuimarisha jumuiya za chama na nafasi ya vijana katika kuimarisha chama pia aliomba wanchama wa ccm kuimarisha harakati za kujenga mafiga matatu katika uchaguzi mkuu wa 2010. Hata hivyo wachunguzi wa mambo wametaja kuwa jitihada za Ridhiwan kutembelea wilaya ni katika kujiimarisha na mchakato wa kuandaa mazingira ya kugombea kupitia vijana kwenye ujumbe wa NEC hivyo kujipa nafasi ya kufahamika kwa wapiga kura kabla ya kufikia kwenye chekeche la uchaguzi.

WAANDISHI WAPATA AJALI IRINGA

Na Danny Tweve, Mbeya. Mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Mbeya NICO MWAIBALE na katibu wake Mkuu Bwana Patrick Kosima wamenusurika kufa katika ajali ya gari iliyotokea leo mchana katika msitu mkuu wa Sao hill Mafinga. Wakisafiria gari aina ya Suzuki Escudo V6 wandishi hao walioambatana na mkewe Nico Mwaibale Bi Laura Njau gari lao lilipasuka gurudumu la mbele na kupinduka mara nne hadi korongoni. Hata hivyo kwa kudra za mwenyezi mungu wote wamenusurika ingawa wana majeraha katika maeneo mbalimbali ya mwili. Inaelezwa na mwaibale kuwa ajali hiyo imetokea wakati akielekea jijini Dar es salaam kujiandaa kwaajili ya kuhamia mkoa wa Tabora ambako amehamishiwa kwenda kuimarisha Timu ya TBC mikoani. Akiwa kwenye eneo hilo inadaiwa gurudumu la mbele lilipasuka na kubiringika mara tatu hadi kwenye korongo ambapo kutokana na msaada wa mikanda waliyokuwa wamejifunga, hawakuweza kupata majeraha makubwa ingawa walibanwa na mikanda mpaka walipookolewa na raia wema. Nico amepongeza ushirikiano uliopatikana kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mfindi Bi Darrly Rwegasira ambaye alipopigiwa simu na wandishi hao aliagiza haraka mganga mkuu wa wilaya pamoja na polisi kutoa gari la wagonjwa na kuweka ulinzi wa kutosha katika eneo la tukio hivyo kupunguza uwezekano wa wizi ingawa wananchi wa eneo hilo walitoa ushirikiano wa kutosha kabla ya msaada wa polisi. Majeruhi wote walikuwa bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya Mafinga.