Ndugu wadau sikuwa hewani kwa muda wa wiki tatu kutokana na kuathiriwa na teknolojia kwani kila nikiingiza password ilikuwa inanikatalia sijui kuna fundi alinifanyia maufndi yake. nimerejea baada ya kutafuta waganga wa fani hiyo
thanks for being patient
indaba2010
Nov 28, 2010
KAMPUNI YA UNYIHA YATOA MSAADA WABATI 100 KUJENGA MABWENI
Mkurugenzi wa Unyiha Associate bwana Charles Chenza akikabidhi hundi yenye thamani ya milioni za kutosha bati 100 kwaajili ya ujenzi wa hosteli katika shule za sekondari wilayanI Mbozi katika mkoa wa Mbeya ambako ndiko alikowekeza. Msaada huo ulipokelewa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Lington Ngaikwela
i ndaba2010
i ndaba2010
TEKNOLOJIA YA UJENZI WA LAMI KWA KUTUMIA NGUVU KAZI HII HAPA
Shirika la maendeleo la JAPAN limetambulisha teknolojia mpya ya ujenzi wa lami kwa kutumia nguvu kazi ambapo majaribio yake yanafanywa katika mkoa wa Mbeya.
zifuatazo hapa ni shemeu ya picha za utekelezaji wa majaribio ya mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Eight Japaniese Engineering Company EJEC
PICHA ZOTE KWA HISANI YA EJEC/JICA

NAUZA GARI KITU CHA KISASA
NAUZA GARI HILO US$15,000 WASILIANA KWA NAMBA YANGU KULIA KWENYE BLOG HII
INATUMIA DIESEL CC 2900 KILOMETA 77,000 IMESHALIPIWA NI KUONDOKA NAYO TU
indaba2010
INATUMIA DIESEL CC 2900 KILOMETA 77,000 IMESHALIPIWA NI KUONDOKA NAYO TU
indaba2010
Nov 18, 2010
UNGA WA BILION 1 MILION 322 WADAKWA BODA YA TUNDUMA
Na Danny Tweve
Mbozi
Watu wawili raia wa Afrika Kusini walikamatwa jana wakiwa na shehena ya madawa ya kulevya yenye thamani ya dola za Kimerekani 822,000 sawa na pesa za madafu za kibongo Bilion 1 Milion 322 wakiwa kwenye mchakato wa kuzivusha kutoka bongo kuelekea Bondeni kwa Mandela.
Akielezea tukio hilo Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Mbeya Rogasian Shirima alisema kuwa walipata dokezo toka kwa raia wema kuhusu kuvushwa kwa madawa hayo na ndipo walipoongeza umakini katika ukaguzi mpakani na kufanikiwa kukamata madawa hayo.
Shirima alimtaja dreva wa gari aina ya Nissan Hardy Board pick up lenye namba za usajili CA 508-650 kuwa ni Vuyo Jack (29) akiwa na mwanamke mwenye asili ya Asia Anastacia Cloete (25) kuwa walibeba jumla ya kilo 42.5 za madawa ya kulevya wakitokea Dar es Salaam na kuelekea Cape town nchini Afrika ya Kusini.
Katika zoezi la upimaji mzigo huo ilibainika kuwepo kwa Cocaine paketi 26 zenye uzito wa kilo 28.5, Heroin paketi 3 za uzito wa kilo 3.5 na Morphine paketi 8 za uzito wa kilo 10.75.
Makasha ya dawa hizo zilipofunguliwa zilikuwa na mihuri ya Pakistan na nembo au chata za Ng’e na nyoka aina ya Cobra ambapo polisi wa kitengo maalum hapo mpakani walipima na kuthibitisha dawa hizo . (chemical identification)
Aidha alama za nyoka na ng’e zimefahamika kuwa ni moja ya vitambulisho vinavyotumiwa na maharamia wa dawa za kulevya kutambulisha dawa aina ya Cocaine na Heroine.
Dereva wa gari hilo Vuyo Jack alipohojiwa juu ya yeye kupakia mzigo huo alidai kuwa yeye aliingia hapa nchini na kwenda Mazimbu Morogoro kwenye kambi ya wakimbizi ambapo alikutana na kundi la watu saba akiwepo mtanzania mwenye asili ya kiasia ambao walimkodi awasafirishie almasi hadi Cape town kwa ahadi ya kumlipa dola za kimarekani 10,000.
“Walidai niwape gari ili wakapakie almasi hizo ambapo walichukua gari hilo wakiniacha Morogoro na kwenda nalo Dar es Salaam ambako walipakia mzigo huo, baada ya wiki moja walinipigia simu kwamba wananiletea gari nianze safari ambapo waliniambia kuwa almasi hizo zimewekwa ndani ya dash bodi” alielezea.
Akielezea zaidi alisema kuwa mhindi ndiye alimwonyesha almasi kipande kimoja na kumwambia kuwa wamepakia nyingi hivyo awe mwangalifu njiani.
Hata hivyo haikuwa rahisi kujua kwa mbinu iliyotumika kwani pakati hizo za madawa ya kulevya yalifichwa kwenye maeneo mbali mbali ya gari ikiwepo kwenye chesesi, mashavu ya gari na maeneo zilimoungiwa taaa za mbele na za nyuma.
Aidha maeneo mengine dawa hizo zilifichwa ndani ya milango, sehemu inayotenganisha AC na rejeta pamoja na kwenye mabomba ya kupitisha hewa ndani ya gati ambapo iliwalazimu wakaguzi kuwaita mafundi magari waliobomoa sehemu mbalimbali za gari hilo na kutoa madawa.
Uchunguzi umebaini kuwepo kwa usafirishaji mkubwa wa dawa za kulevya kutokana na mbinu kubwa ya wafanyabiashara hao ambao maafisa wa TRA siyo rahisi kung’amua.
mwisho
indaba2010
Nov 15, 2010
salam za OB kwa JK
Rais wa Marekani,Barrack Obama
Kwa niaba ya Marekani, Ninawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha uchaguzi mkuu hivi karibuni na kuendeleza utamaduni wenu wa kuendesha chaguzi za vyama vingi toka mwaka 1992.
Ninatarajia kufanya kazi na Rais Jakaya Kikwete na wabunge wa Bunge la Kumi tunapoendelea kujenga na kuimarisha ubia wa muda mrefu na wenye mafanikio kati ya mataifa yetu katika kuendeleza malengo ya pamoja ya maendeleo na kukabiliana na changamoto nyingi za kimataifa zinazotukabili.
Aidha, ninatoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad, serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa na zaidi sana kwa watu wa Zanzibar ambao wameweka historia kwa kufanya uchaguzi wa amani baada ya miaka kadhaa ya chaguzi zilizogubikwa na machafuko.
Kama nilivyomueleza Rais Kikwete nilipokutana naye katika Ikulu ya White House hapo mwaka 2009, Watu wa Marekani wanawaunga mkono Watanzania wote katika jitihada zenu za kuimarisha utawala wa kidemokrasia na uwazi, kutumia kikamilifu fursa za Muungano wenu na kuhakikisha kuwa hatua mlizopiga na mafanikio mliofikia katika kujenga amani na ustawi wa kudumu hayarudi nyuma.

Nov 9, 2010
WATOTO WANNE WAJIFICHA UVUNGUNGI MWA HOOD NA KUSAFIRI HADI DAR
Basi la Abood lenye namba za usajiri T542 AZE limenusurika kupata ajali jana baada ya Watoto wane wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya, kujificha na kukalia mdumowa breki kwenye chesisi ya basi hilo na kusababisha mfumo wa breki kushindwa kufanya kazi.
Habari kutoka kwa mmoja wa abiria waliosafiri na basi hilo Bwana Edmund Makombe na kuthibitishwa na kondakta wa basi hilo bwana Ayoub Nassoro, Watoto hao walikuwa wamejilaza kwenye mfumo wa breki na wengine kwenye chasis.
Imeelezwa na watoto hao kuwa walipanda waliingia kwenye basi hilo alfajiri katika kituo kikuu cha mabasi cha Mbeya na kujificha uvunguni kwenye chasis ambapo mmoja wao alijilaza kwenye waya za breki, na kwamba wakiwa karibu na hotel ya aljazeera iliyopo Ruaha Mbuyuni walishitukia dereva akisimamisha gari kwenye moja ya maeneo yanayofanyiwa matengenezo.
Kwa mujibu wa Kondakta wa basi hilo Ayoub Nassoro maarufu kama Nyerere , anasema wakati gari limesimama kwaajili ya kusubiri magari kupishana alienda kuchungulia uvunguni kwaajili ya kuangalia hali ya tairi na ndipo alipowakuta watoto wawili wakiwa wamekilaza kwenye difu ya nyuma.
Anasema kuwa baada ya kuwatoa hao wawili, walimweleza kuwa wapo wengine uvunguni humo na katika kuchugulia wakawakuta kwenye chasis huku mmoja akiwa ameshikilia waya za mfumo wa breki.
Watoto hao wamejitambulisha kwa majina ya Frank John (12), Fabi Yusuph (12), Christopher Tweve (10) na Yohaba Robart (12) wote wakazi wa Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Wakizungumza katika hoteli ya Aljazeera ambako walinunuliwa chakula na wafanyakazi wa kampuni ya Abood na baadaye kuachwa ili warejeshwe mbeya na mabasi yanayoelekea Mbeya , wamesema sababu za kurtoroka kwao ni kutokana na hali ngumu ya maisha na kwamba walitegemea kwenda Dar es salaam kutafuta maisha.
Wanadai kuwa tayari kuna wenzao ambao wameshasafiri kwa utaratibu huo na kwamba hawana mawasiliano ingawa wanaamini wapo Dar es salaam na huenda wana maisha mazuri ndiyo sababu wakashawishika nao kwenda huko.
Licha ya kondakta kuelezea kuwa gari lilisimama katika utaratibu wa kawaida wa kulichunguza, mmoja wa abiria ambaye alikuwa karibu na kiti cha dereva anaeleza kuwa alimsikia dereva akimwelekeza kondakta huyo aangalie kwenye mfumo wa breki baada ya kubaini kuwa mzito tofauti na siku zingine.
Anaesema akiwa anaagalia uvunguni alibaini kijana huyo akiwa amejilaza kwenye waya wa breki na ndipo alipotoa taarifa kwa dereva kuwa kuna watu uvunguni.
Mashuhuda wa tukio hilo wameonekana kushangazwa na ujasiri wa watoto hao ambao wakati wakitolewa uvunguni walikuwa wamechafuka sana kutokana na vumbi la uvunguni kuwatanda usoni huku wakiwa wamechoka.

Nov 4, 2010
WALIOTEMBEZA JENEZA TUNDUMA WATINGA MAHAKAMANI
Vijana wawili wamepandishwa jana kwenye Mahakama ya mwanzo ya Vwawa wilayani Mbozi kwa kosa la kutembeza jeneza lililofunikwa bendera ya chama cha mapinduzi pamoja na msalaba katika mji mdogo wa Tunduma baada ya kutangazwa ushindi wa kiti cha ubunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA jimbo la Mbozi Magharibi.
Waliopandishwa kizimbani ni Selemani Ibrahimu maarufu kama mwarabu na Maneno Halongo wote wakazi wa mji wa Tunduma.
Wakisomewa shitaka lao mbele ya Mh hakimu wa mahakama ya mwanzo Vwawa Ismail Karuta, mwendesha mashitaka wa polisi koplo Pascal Mkondya aliieleza mahakama kuwa mnamo Novemba 2 mwaka huu saa 7 mchana katika mji wa Tunduma watuhumiwa walibeba sanduku mfano wa jeneza na bendera ya CCM wakiimba nyimbo za mazishi kitendo ambacho kilikuwa cha uvunjifu wa amani.
Alisema chini ya sheria ya maadili ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani namba 124 ya 1985 sura ya 342 kifungu kidogo cha 2 d pamoja na tangazo la serikali namba 273 la agosti 2010 ambalo linakataza vitendo vyenye lengo la kudhalilisha ama kukikashifu chama kingine.
Pamoja na kukana shitaka hilo, washitakiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana baada ya hakimu Ismail Karuta kuwataka kudhaminiwa na watu watatu ambao ni watumishi wa serikali pamoja fedha kwa maneno kiasi cha shilingi 500,000/=. Watuhumiwa walipelekwa mahabusu hadi novemba 17 kesi yao itakapoanza kusilikilizwa.
Danny tweve Mbozi

Nov 2, 2010
CHADEMA YAVUNA UBUNGE MBOZI MAGHARIBI, CCM MBOZI MASHARIKI
Na Danny Tweve Mbozi.
Matokeo ya ubunge katika majimbo mawili ya Mbozi mashariki na Magharibi yanaonyesha vyama vya CCM na CHADEMA kugawana majimbo.
Wakati chama cha Mapinduzi kikichukua jimbo la Mbozi Mashariki kupitia mgombea wake Godfrey Zambi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimechukua jimbo la Mbozi Magharibi kupitia Mgombea wake David Silinde.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa majimbo hayo mawili Bw. Levison Chillewa ametangaza kuwa kwa jimbo la Mbozi Mashariki Godfrey Zambi wa CCM amepata kura49,095, wakati Allamis Mwampamba (CHADEMA) kura 31,997 na Nkunyutila Siame kupitia CUF amepata kura 839.
Kwa upande wa jimbo la Mbozi Magharibi Msimamizi huyo alimtangaza David Silinde CHADEMA baada ya kupata kura 20835, huku mgombea wa chama cha mapinduzi Dr Luka Siame akipata kura 20,203 na kasabuni Asukile ca CUF akiwa na kura 220.
Kwa upande wa madiwani jimbo la Mbozi mashariki CCM imechukua viti 16 kati ya 18 vilivyopo huku viti viwili vikienda CHADEMA kwa miji ya Vwawa na Mlowo. Jimbo la Mbozi magharibi CCM imeshinda viti 12 vya Udiwani na ChADEMA viti viwili ( 2) vya miji ya Tunduma na Ndalambo.
MWISHO