Adverts

Jul 13, 2013

wanaume Mbozi wajitokeza wengi kuondoa mikono ya sweta


Wanaume 4,682 walipata huduma  ya tohara katika wilaya Mbozi katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu imefahamika.

 Hayo yalitolewa katika taarifa ya Mganga mkuu wa wilaya ya mbozi katika taarifa yake katika kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa huduma ya  tohara  kwa wanaume

Wilaya ya Mbozi kabla ya zoezi hilo  ilikadiliwa kuwa ilikuwa chini ya asilimia 60 ikilinganishwa na maeneo mengine

 Kulingana na tafiti zilizofanywa huduma hii ya tohara kwa wanaume imepunguza uwezekano wa wanaume kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi ukilinganisha na wanaume wasiofanyiwa tohara.

 Taarifa ya mganga mkuu wa wilaya ya mbozi inaonyesha mafanikio haya ni sehemu ya mpango wa uhamasishaji jamii uliofanywa kupitia radio na mikutano ya hazara

 Kulingana na taarifa hiyo ina sema mwanaume asiye tahiriwa  anapofanya tendo la ngono kuna uwezekano wa  kupata michubuko kwa hurahisi hambayo ni rahisi  kwa virusi vya ukimwi kupenya kwa urahisi

Aidha unashauriwa kuwa tohara ifanyike  katika mazingira safi na salama pia ifanyike katika jamii kama njia mojawapo  ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Huduma hii ya tohara inashauriwa ifanyike katika hospitali na wataaramu wa afya daktari  au tabibu  kwa usalama ilikupunguza madhara mbalimbali yanayo weza kutokea

Hivyo jamii inapaswa ifahamu kwamba kuna uhusiano  makubwa kati ya tohara nakupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.

 

 

 
Na Anjela Kivavala DSJ