Na Anjela Kivalala DSJ
Aga khan foundation wakishirikiana na serikali wapo mbioni kutekeleza
mradi wa tuunganishe mikono pamoja unaolenga kuboresha afya ya mama mjamzito na watoto nchini.
Aidha mradi huo unalenga kuboresha mfumo wa rufaa kwa wagonjwa,kujenga
uwezo na huduma za afya kwa mama mjawazito na watoto
Kulingana na taarifa
iliyotolewa na mfuko huo, Mradi huo pia unakusudia kuboresha kiwango cha upatikanaji wa huduma ya afya kwa
mama mjamzito na watoto, kuongeza kiwango cha matumizi ya huduma ya afya .
Kaulimbiu ya mradi huo wa tuunganishe mikono pamoja inatafsiriwa kuwa ‘’hakuna mwanamke ambaye atafariki wakati
wa kujifungua na hakuna sababu yoyote ya
mtoto kufariki kwa magonjwa yanayo
zuilika’’. Inafafanua sehemu ya taarifa hiyo
Mpango wa mradi huo wa tuunganishe mikono pamoja utatekelezwa katika mikoa mitano
ya Mwanza Dodoma Iringa
Mbeya na morogoro ili kuboresha afya ya
mama mjamzito na watoto.
Kulingana na taarifa
iliyotolewa na Aga khan health services,
utekelezaji wa mradi huo utafanyika katika
kipindi cha miaka mitatu kuanzia Juni 2013 kwa mikoa mitano nchini Mbeya ikiwa
miongoni mwake na wilaya za Mbozi, Kyela na Mbeya zikihusika kikamilifu.
Mradi huo unafadhiliwa
na shirika la maendeleo la Canada -CIDA ambapo utekelezaji wake utashirikisha mashirika
mengine yakiwemo AKHST, AKU na wadau wengine katika jamii huku wizara ya
afya na ustawi wa jamii pamoja na Aga Khan Foundation wakiwa wasimamizi wa kuu
wa program hiyo.