Adverts

Jul 9, 2013

CHILIPAMWAO WAJITOSA KUWEKA MJI WA TUNDUMA KATIKA HALI YA USAFI



 miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na kikundi cha CHILIPAMWAO katika mji wa Tunduma kuwezesha usafi katika kituo cha afya ambacho kimekuwa kikitoa huduma kwa wakazi wa Tunduma pamoja na watu kutoka upande wa pili wa Mpaka yaani Zambia
Mwenyekiti wa Kikundi cha CHILIPAMWAO  bwana Kulwa Nyondo akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa uongozi wa kituo cha afya  Tunduma, aliyevaa koti la suti ni diwani wa Kata ya Tunduma Mh Frank Mwakajoka

Wanakikundi wa CHILIPAMWAO wakifanya usafi katika mazingira yanayozunguka kituo cha afya cha Tunduma- (Picha zote   na Anjela Kivavala wa dsj)


Na  Angela Kivavala dsj
Halmashauri ya mji mdogo Tunduma imekipongeza kikundi cha wazawa wa mji huo “Chilipamwa” kwa kujitolea katika kufanya usafi katika kituo cha Afya
Diwani wa halmashauri ya mji mdogo Tunduma Ndugu Frank Mwakajoka awapongeza wa zawa  wa mji mdogo kwa kujitolea kusafisha na kufanya usafi katika kituo cha Afya Tunduma
“natoapongezi kwenu kwa kujitolea kwa hali na mali na kwa uzalendo kuupenda mji wenu kwa kujitolea kufanya usafi kwenye kituo chetu cha afya na huu uwe mfano wa kuigwa vikundi vingine” alifafanua bwana Mwakajoka.
Pia aliwaomba  vikundi vingine kuiga mfano kutoka kwa kikundi cha Chilipamwao kwa kujitolea kukisaidia kituo hicho cha afya cha Tunduma pamoja na kushiriki katika shughuli zingine  za maendeleo.
Mwenyekiti wa kikundi hicho cha wazawa wa Tunduma  ndugu Kulwa Nyondo alisema kuwa kipindi kirefu hakuja kuwepo mfumo wa wananchi kujitolea katika shughuri za maendeleo
“tumeamua kujitolea kufanya usafi katika kituo chetu cha afya kwani tumeona usafi au lidhishi na vifaa havikidhi mahitaji katika kituo chetu” alisema bwana Nyondo
Aidha aliwaushukuru uongozi wa kituo cha afya  Tunduma kwa kukubali ombi lao la kujakufanya usafi  katika kituo hicho  na kwamba huo ni mwanzo tu  na kwamba wataendelea kujitolea hata katika shughuli zingine za maendeleo katika mji wa Tunduma
Kikundi hicho cha wazawa kilijitolea vifaa vya kufanyia usafi vyenye thamani ya 1.5 mililioni ikiwa ni pamoja na kubadili taa katika wadi na kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kituo hicho cha afya.