Na Angela Kivavala DSJ
Halmashauri
ya Wilaya ya mbozi iko katika mchakato wa kuomba kuongeza kata na vijiji vipya
ili kusogeza huduma karibu na wanainchi.
Kata
zipatazo sita (6) zinategemewa kuanzishwa
na vijiji 24 baada ya mapendekezo hayo kuwasilishwa ofisi ya Waziri mkuu
Tamisemi
Wilaya ya Mbozi ina watu 446,339,Asilimia 88% ya Wakazi wake hujishughulisha
na kilimo ambacho huchangia asilimia 80% ya pato la Wilaya.
Hayo yalisemwa
mwishoni mwa wiki katika Maadhimisho ya Siku ya Serikali
za Mitaa ambayo hufanyika Julai mosikila mwaka.
Lengo la
sherehe hizo ni kutoa mwanya kwa jamii kutambua na kuzifahamu shughuli na
huduma mbali mbali zinatolewa na Taasisi za Serikali za Mitaa yaani halmashauri za Majiji, Manispaa na wilaya.
ujumbe
wa mwaka huu ni “Amani, Uadilifu na Uwajibikaji kwa wote ni Nyenzo muhimu
katika mchakato wa Katiba mpya na Ustawi wa Serikali za Mitaa”
Halmashauri
ya Wilaya ya Mbozi inaendelea kusimamia utekelezaji wa mabadiliko ya katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tuko kwenye mchakato wa kupitia Rasimu ya
Katiba iliyotolewa kwa kutumia mabaraza ya Kata yaliyochaguliwa yalisomwa katika
hotuba kwa wananchi wa mbozi.
Katika
kipindi cha mwaka moja uliopita Halmashauri iliajilia wa tumishi wapya 410 kati
yao walimu wa sekondari ni 210 na washule za msingi nio 182 na watumishi wa
afya ni 10 ambapo kwa kiasi kikubwa ufanisi wa kazi umeongezeka katika utoaji
wa huduma kwa wananchi wa mbozi
Wilaya
ina jumlayashule za sekondari 40za selikari ambapo kati ya shule hizo ni shule
1 tu yenye kidato cha tano na sita Halmashauri ya wilaya ya mbozi iko kwenye
mchakato wa kuanzisha shule za kidato cha tano na sita katika kata tofauti.