Wanaume 4,682 walipata
huduma ya tohara katika wilaya Mbozi
katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu imefahamika.
Hayo yalitolewa katika taarifa ya Mganga mkuu
wa wilaya ya mbozi katika taarifa yake katika kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa
huduma ya tohara kwa wanaume
Wilaya ya Mbozi kabla
ya zoezi hilo ilikadiliwa kuwa ilikuwa chini
ya asilimia 60 ikilinganishwa na maeneo mengine
Kulingana na tafiti zilizofanywa huduma hii ya
tohara kwa wanaume imepunguza uwezekano wa wanaume kupata maambukizi ya virusi
vya ukimwi ukilinganisha na wanaume wasiofanyiwa tohara.
Taarifa ya mganga mkuu wa wilaya ya mbozi
inaonyesha mafanikio haya ni sehemu ya mpango wa uhamasishaji jamii uliofanywa
kupitia radio na mikutano ya hazara
Kulingana na taarifa hiyo ina sema mwanaume
asiye tahiriwa anapofanya tendo la ngono
kuna uwezekano wa kupata michubuko kwa
hurahisi hambayo ni rahisi kwa virusi
vya ukimwi kupenya kwa urahisi
Aidha unashauriwa kuwa
tohara ifanyike katika mazingira safi na
salama pia ifanyike katika jamii kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Huduma hii ya tohara
inashauriwa ifanyike katika hospitali na wataaramu wa afya daktari au tabibu
kwa usalama ilikupunguza madhara mbalimbali yanayo weza kutokea
Hivyo jamii inapaswa
ifahamu kwamba kuna uhusiano makubwa
kati ya tohara nakupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.