Adverts

Jan 28, 2011

ASKOFU DKT MDEGELLA ASEMA BARAZA LA MAWAZIRI BADO HAJALIONA...

ASKOFU DKT MDEGELLA ASEMA BARAZA LA MAWAZIRI BADO HAJALIONA...: "
ASKOFU wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Iringa Dkt Owdenburg Mdegella (pichani)amedai kuwa utendaji mbovu wa baraza la mawaziri la serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Jakaya Kikwete umekuwa unatokana na mawaziri na viongozi kufanya kazi kwa kutegeana . Pamoja na hali hiyo bado amesema kuwa ipo hatari ya maendeleo ya Taifa kuyumba zaidi iwapo chama cha mapinduzi (CCM) kitaendelea kuwepo madarakani na watendaji wa chini kuendelea kumdanganya Rais kwa ajili ya kuonekana wema. Dkt Mdegella amesema kuwa ili nchi kurudi katika heshima yake ni vema azimio la Arusha kurudishwa ambalo litasaidia kumaliza ufisadi nchini na kuondoa tofauti ya serikali na mawaziri wake. Dkt Mdegella aliyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na gazeti hili kuhusiana na mwenendo wa serikali iliyopo madarakani na sakata la malipo ya dowansi ambayo kwa upande wake amesema kuwa malipo hayo ya dowansi na danganya toto na kuwa serikali italaumiwa zaidi iwapo itakubali kulipa malipo hayo hewa. Pia Dkt Mdegella alisema kuwa kasi ndogo ya utendaji kazi kwa baraza la mawaziri umeanza kuwakatisha tamaa wananchi na kuwa ni vema baraza hilo la mawaziri kuongeza kasi zaidi ya utendaji ili kuharakisha kasi ya maendeleo kwa wananchi badala ya mawaziri kuendelea kufanya kazi za chama tawala pekee na kukitetea kwa uovu unaofanyika. Hata hivyo alikitaka chama tawala kukaa chini na kukinusuru chama hicho kwa kuwapata wabunge wasema kweli daima ambao watafikisha ukweli wa mambo kwa mwenyekiti wa chama hicho na Rais Kikwete badala ya ilivyosasa kila kiongozi anataka kuonekana mwema kwa Rais na kueleza mazuri pekee na kuacha kufikisha ukweli kwa maana ya hali halisi ya nchi inavyokwenda. DKt Mdegella alisema kwa upande wake haweze kutabili kama baraza la mawaziri la sasa litavunjwa ama lah na japo anachokiona sasa ni kushindwa kazi kwa baraza hilo la mawaziri hasa waziri wa nishati ambapo gharama za umeme zimezidi kupaa bila wizara husika kuonyesha uhai wake wa kushusha bei hizo. 'Mawaziri wengi wa Rais Kikwete wamekuwa wakifanya kazi ya kujipendekeza kwa Rais ....sasa hofu yangu mimi Taifa linaendelea kuyumba ....ila napenda kusema mimi si mtabiri kama Shekh Yahaya ambaye amekuwa akitabili ila naeleza kutokana na uhalisia wa mambo yanavyokwenda sasa Alisema kuwa sehemu kubwa ya mawaziri wamekuwa wakionyesha kuogelea katika nafasi zao na kuwa iwapo mambo yataendelea kuwa hivyo nchi inazidi kuyumba zaidi . Pia alisema kuwa matamko mbali mbali yanayoendelea kutolewa na CCM kupitia jumuiya zake ni kielelezo tosha kuwa chama hicho kinazidi kufilisika sera na maadili ya CCM ambayo wengi waliyazoea yameonyesha kuyumba zaidi . Katika hatua nyingine askofu huyo aliionya serikali kuacha mara moja kuzuia wananchi kufanya maandamano ya kuipongeza ama kuipinga serikali yao kwani kufanya hivyo ni kuzidisha jazba kwa wananchi na kusababisha makubwa zaidi kama ilivyotokea Arusha. MWISHO
"