Adverts

Jan 20, 2011

DEREVA AJISALIMISHA POLISI

Dereva Dankel Mwamasika aliyesababisha kifo na vurugu zilizotokea leo jioni katika kijiji cha Ihanda amejisalimisha kituo cha Polisi cha Vwawa baada ya kufanikiwa kuchoropoka kabla ya basi alilokuwa anaendesha kuchomwa moto.
Dereva huyo amedai kuwa alidandia kwenye coaster iliyokuwa nyuma yake na kwenda moja kwa moja kituo cha Polisi cha Vwawa kujisalimisha.
Hatua hiyo imewezesha kutambulika kwa namba za gari ambazo hazikuwepo kwenye gari hilo kutokana na wananchi kugombaniana kama mpira wa kona na kulichoma moto na kubakia majivu.