Adverts

Jan 15, 2011

Jumuiya Ya Wanataaluma UDSM Waijadili Katiba Mpya

Jumuiya Ya Wanataaluma UDSM Waijadili Katiba Mpya: " 1.Waendeshaji wa Mdaharo wa kujadili swala la Katiba mpya ya Tanzania kwa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA),toka kushoto ni Prof. Issa Shivji,Dr. Kitila Mkumbo pamona ja Ndg. Jenerali Ulimwengu wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wajumbe wa mdaharo huo mchana huu katika ukumbi wa Nkurumah,Chuo kikuu cha Dar es Salaam. 2.Prof. Issa Shivji azungumza katika Mdaharo huo huku akinukuu baadhi ya maneno yaliyokuwa yakitamkwa na Hayati Mwl. Nyerere kuhusiana na swala la Katiba Mpya.Mdaharo huu umemalizika hivi punde katika ukumbi wa Nkurumah ulipo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mchana huu. 3.Baadhi ya Wanataaluma na wanasiasa wakongwe wakifuatilia Mdaharo huo. 4.Mmoja wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Mzee Ibrahim Kaduma akichangia mada zilizokuwa zikutolewa na baadhi ya wajumbe waliohudhulia Mdaharo huo kuhisia na swala la kupatikana kwa Katiba mpya ya nchi yetu.
" new post