Pichani ni wanachama wa kikundi cha wanaoishi na virusi vinavyosababisha UKIMWI kijiji cha Iporoto, kwa uwazi wamejitokeza na kuomba picha hii iwekwe kwenye blog hii kwamba wanamatatizo ya lishe na kikundi chao hakina support yoyote, wamekuwa wakisikia tu kuwa vikundi vya waviu baadhi ya maeneo nchini vinapata misaada kutoka kwenye mifuko mbalimbali na taasisi za biashara lakini vijijini hawafikiwa kabisa na matokeo yake wanakufa tu! maneno haya yameniingia nami kama mdau wao ninatangaza fulsa hii kutafuta wadau na mashirika yanayojitolea kuona namna yanavyoweza kuwafikia watu kama hawa na kufanya nao kazi. kwa ujumla kikundi hiki kimeeleza matatizo kuwa hata kupima CD4 baadhi ya wanachama wake wana miaka mitatu hawajapima kwa kuwa wakienda wanaambiwa mashine inapima watu 50 tu kwa siku sasa nauli za kurudia rudia hospitalini zinakosekana!.,Wengine wanaeleza kuwa wamekuwa wakikosa dawa za kutibu magonjwa nyemelezi hata septrine ambazo ni muhimu kwao hazipatikani kabisa! Pia wana Kuku wawili tu waliosaidiwa kama kikundi, hivyo wadau kama una kamsaada ka kukanzisha miradi kwao basi unaweza kunikong'olia nikakuunganisha nao halafu nitatoa hata publicity bureee kabisa!
Tupo pamoja wanakikundi mungu ni mwema atawafanyia msiyoyategemea, manake wapo watanzania wenye mapenzi mema na ninyi, karibuni muwatembelee hata kuchangia kwa chochote, mawazo na mali ili kikundi hiki chenye watoto nane wanaoishi na VVU waweze kuendelea kutoa mchango wao katika taifa letu la Tanzania.