Adverts

Jan 14, 2011

Kitabu Cha JK Chazinduliwa Ikulu

Kitabu Cha JK Chazinduliwa Ikulu: "
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Wasifu wa Maisha yake, akishuhudiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mwandishi wa kitabu hicho Profesa Julius Nyang'oro leo mchana Ikulu, Dar es salaam
Rais Kikwete akionyesha vitabu viwili (cha kiingereza na kiswahili) kwa wageni waliohudhuria hafla hiyo wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho tarehe 9 Desemba 2010 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwandishi wa kitabu cha wasifu wake na kuwasihi wana taaluma na watanzania wengine kuandika vitabu ili historia ya nchi yetu isipotee. Rais Kikwete ameyasema hayo wakati akizindua kitabu chake kilichoandikwa na Profesa Julius Nyang'oro.
Mwandishi wa Kitabu cha Wasifu wa JK Profesa Julius Nyang'oro akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua kitabu hicho ambacho alikiandika na kuelezea sababu mojawapo iliyomfanya aandike kitabu hicho ni kutokuwa na kitabu cha aina hiyo kwa viongozi wetu wa nchi isipokuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Profesa Rugarabumo akitoa tathmini ya Kitabu cha JK wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kitabu hicho, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 9 Desemba 2010.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wakiongea na Profesa Nyang'oro ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha Wasifu wa JK wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Shukuru Kawambwa.
Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akizungumza na Bi. Amina Mtengeti ambaye ni Shangazi wa Profesa Nyang'oro mwandishi wa kitabu cha JK wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Pichani ni viongozi wengine wa kitaifa na marafiki wa Profesa Nyang'oro waliohudhuria uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Ikulu Bwana Michael Mwanda (wa tatu kutoka kulia safu ya waliokaa) akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Profesa Nyang'oro Bi. Emma Kasiga aliyehudhuria uzinduzi wa kitabu cha JK uliofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanafamilia ya Mheshimiwa Rais Kikwete wakiperuzi kurasa za kitabu cha Wasifu wa JK kilichozinduliwa leo Ikulu Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Bwana Beno Malisa akizungumza na Miraji Kikwete kwenye uzinduzi wa Kitabu Cha Wasifu wa JK Ikulu jijini Dar es salaam.
Nakala ya kiingereza ya Kitabu cha Wasifu wa JK kama kinavyoonekana. Picha ya chini ni Profesa Nyang'oro akitia saini nakala za kitabu hicho zilizogaiwa bure kwa wageni wote waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo. Vitabu hivyo vitaanza kuuzwa kwenye duka la vitabu la Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kuanzia kesho tarehe 10-12-2010 kwa gharama ya shillingi 25,000/=
" new post