Habari toka kwa ripota wetu huko Dodoma zinasema Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanda Pinda aka 'Mtoto wa Mkulima' amewasili Chuo Kikuu cha Dodoma mchana huu na hivi tunavyoongea anapita kila mahali ukagua majengo na miundombinu ya chuo hicho asmbacho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 40,000.
Mh. Pinda, huku akishangiliwa na wanafunzi na waalimu ambao wanaonesha kufarijika kwa ujio wake ambao huenda ukaondoa kwikwi kibao zinazowakabili, amepitia mabweni, madarasa na hata vyoo na kujionea hali halisi. Inatarajiwa ataongea na wanafunzi na wafanyakazi mwishoni.
stay tuned!
" source: michuzi blog
new post