Adverts

Jan 15, 2011

TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO…

TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO…: "

VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo.

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.

Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.

  1. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
  2. Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic

Jambo la kuangalia ni je?

  1. Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
  2. Umeinama au umelala
  3. Ukishakula chakula

Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.

Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka.

Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.

Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.

Hasa kama hunywi maji.

Soma zaidi suala hili hapa:

http://kitoto.wordpress.com/2010/04/13/njia-kumi-kusaidia-kupunguza-unene/

Kama unapatwa kichomi ukiwa umelala au umeinama ina maana kuna tatizo pia la mzunguko wa damu ndani ya moyo au kwenda moyoni. Labda una tatizo la unene (je unafanya mazoezi ya kutosha?) kama unafanya mazoezi, je unafanya mazoezi ya aina gani?

Kuna mazoezi ya aina mbili.

Mazoezi ya nguvu na haraka (cardio vascular); kama kukimbia, mpira, ngumi, kuinua vyuma nk.

Au mazoezi laini yanayofanywa kwa kukihimili (isometric) mathalan ukiweka mkono upande mmoja wa kichwa huku ukisukuma kichwa kisukumane na mkono, unafanya tizi la kuongeza nguvu ya shingo. Zoezi aina hii linaitwa Isometric.

Aina ya mazoezi ya aina hii ni kama Yoga, Pilates na baadhi ya mitindo mbalimbali ya mapigano yaani masho ati mathalan Tai Chi ya Kichina.

Tizi la Yoga zuri sana maana limetulizana:

Tai Chi

Pilates si tofauti sana na Yoga ni kama ndugu wa karibu. Ila Pilates inafafanua zaidi mambo mengine kama tumbo nene:

AinNI muhimu kuchanganya mazoezi haya mawili. Yaani ukishafanya mazoezi ya nguvu, ya kuhema unatulizana.

Kama una kichomi cha mara kwa mara yaweza kuwa ni dalili za ugonjwa wa moyo, kisukari au mambo mengine. Kuondokana na mambo haya:

  1. Kamwone mganga wa moyo
  2. Kama huna ugonjwa wa moyo angalia unavyokula. Je, unakula sana vyakula vya mafuta
  3. Punguza ulaji wa mafuta au vyakula vizito jaribu kula zaidi samaki ambao huwa na mafuta yasiyoumiza mwili.
  4. VITUNGU SAUMU VIBICHI vinasaidia sana kukinga moyo, matatizo ya mafuta, lakini tatizo ni harumu mbaya ya mdomo. Hivyo unaweza kuwa unachanganya na mboga nyingine za saladi unapokula mlo kila siku. Kama nyanya, matango, nk.

Mbali na ulaji suala la mapumziko ya kutafakari au kwa kimombo Meditation limefanyiwa utafiti na kuonekana kwamba linasaidia sana maradhi ya moyo, akili na “stress” ya mwili kwa ujumla. Jaribu hizi hapa chini, ukiweza dakika kumi hadi 20; mara mbili kwa siku, kufuatana na muda ulio nao.

1.KUKAA TU

2. KUVUTA PUMZI

http://www.youtube.com/watch?v=-j5Z4E2wkh4

3. KULALA CHALI HUKU UNAVUTA NA KUPUMUA…hii ni aina ya masho ati ya Kirusi ambayo inasisitiza Uvutaji pumzi sahihi.

Inaitwa Systema.

Jisomee zaidi habari kuhusu vyakula vinavyouboresha na kuukinga mwili hapa:

http://him.uk.msn.com/health-and-fitness/articles.aspx?cp-documentid=155013085

" new post