Meza kuu wakiitikia dua, kutoka kulia mwenye miwani ni mwenyekiti wa madrasa sheirk Amran Rashid, akifuatiwa na mgeni rasmi ustaadh Suphian Masasi, anayefuata kulia kwa mgeni rasmi ni mratibu mkuu wa madrasa \Mufti Haji (mwenye bargashia) na anesoma dua mwisho kushoto ni mwalim mkuu wa madrasa ustaadh Hakim
Wa kwanza kulia mwenye shati ya mistari ni ustaadh Mudhuhir akiwa na baadhi ya wazazi wa wanafunzi wakiitikia dua maalum
Wanafunzi wa madrasa wakifuatilia kwa mazingatio mawaidha maalum yaliyotolewa na mwalim mkuu wa madrasa ustaadh Hakim
Wanafunzi wa ngazi ya masahafu kuanzia juzuu ya tatu (3) hadi juzuu ya kumi (10) wakidurusu na kutafsili baadhi ya Aya kulingana na sura aliyofikia kila mmoja wao. mbele ya wazazi na wageni waalikwa.
Asalaam aleykum kaka Michuzi na wasomaji wote wa Globo hii,
Tuanze kwa kumshukuru Allah Subhana wataalah kwa kutujaalia, afya na uhai kufikia hapa tulipo leo hii. Pili Allah aijalie globo hii maendeleo yenye kukuza upendo, amani, ushirikiano na furaha kwa wasomaji wote wa globo hii 'INSHAALAH'
Sisi ndugu zenu wa Madrasat Muhamad ya hapa LEEDS tuliandaa sherehe maalum ya kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi wote waliomaliza juzuu Amaa katika muhula huu, na kwamba kuanzia tarehe 05.01.2011 mwanzo wa muhula mpya ujao, wanafunzi hawa wataanza kusoma Masahafu.
Sherehe ziliandaliwa katika ukumbi wa madrasa wa Ebbo Garden Leeds Mjini zilianza saa 3.30 Asubuhi mpaka saa 6.30 mchana, Sherehe ziliadhimishwa kwa usomaji wa kuraan wa aina mbalimbali kwa wanafunzi wahitimu na wanafunzi wakongwe. Mawaidha kutoka kwa mufti Haji na ustaadh Hakim yalikuwa ni sehemu kuu ya msingi na muelekeo wa sherehe yenyeweri wa .
Na mwisho kabisa wahitimu hawa wadogo wenye wastani wa umri wa miaka 7 walizawadi bahasha maalum kila mwanafunzi. Mgeni rasmi katika sherehe hii alikuwa Ustaadh Suphian kutoka chuo kikuu cha Leeds.
Tunawaombea dua vijana wote waliofanikiwa kufikia hatua hii. INSHALLAH , waendelee na masomo zaidi na waje kuwa mwanga wa amani na taa ya umoja, furaha na upendo katika jamii. Na wewe neema kwa wazazi wao na jamii yote kwa ujumla.
Afya njema, Amani, furaha na upendo kwako wewe Issa wa Michuzi na wasomaji wote wa globo hii
Asalaam Aleykum
Amran Rashid (mwenyekiti)
na
Sheirk Khasim Mintonde (Katibu).
"