Huwezi kuamini eneo hili lipo upande wa Zambia lakini Mbolea ya Urea yenye mifuko ya Tanzania inauzwa hapa!!! hii ndiyo black Market bwana!!!!!
Huu ndiyo mtaa wenyewe wa Black Market ambapo asilimia 90 ya bidhaa zake hazilipiwi kodi na TRA wanadaiwa kusurender kwani wakati wakitaka kukamata bidhaa ambazo hazijalipiwa ushuru, watu hurukia upande wa pili hivyo kuhitaji askari wa upande wa Zambia wasaidie kaazii kweli kweli!!!!!
Black market forever huku hata maini ya Bundi yanapatikana kwa jinsi bidhaa nyingi zinazosakwa maeneo mengine kama vipodozi vilivyopigwa marufuku vinapatikana hapa, tena wazi wazi hata bila kuhitaji lugha za uficho, pia viloba ama pombe kali za kutoka malawi na zambia kama power nk zipo za kumwaga tena kwa bei ya jumla!!!!!!!!!!!!