CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) kimezindua mkakati wake wa kuwachochea wananchi kuiondoa Serikali kwa nguvu kama walivyofanya wananchi wa mataifa ya Tunisia, Misri, Libya na Baharin kinyume na Katiba ya Nchi.
"
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa na baadhi ya wabunge wake katika uwanja wa furahisha Jijini Mwanza, walisema kuwa CHADEMA haikubaliani na serikali ya CCM pamoja na kueleza kutomtambua Rais Jakaya Kikwete kuwa ni kiongozi wa taifa hili na badala yake kuvunja katiba na kudai Dk.Willbrod Silaa kuwa ndiye Rais ambaye hakutangazwa.
Akiwahuhutubia maelfu ya wananchi katika uwanja huo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe, alisema kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli ambazo serikali ya Kikwete na CCM wamekuwa wakizibeza na kuwakejeli hivyo wamefika Mkoani Mwanza kuungwa mkono na nguvu ya umma ili kuiondosha Serikali hiyo madarakani serikali .
“Tumekuja kwenu kuomba kibali cha kuhakikisha mnatuunga mkono ili kuiondosha serikali ya CCM pamoja na Kikwete na hivyo tunaanzia mwanza kuzindua mkakati huu wa kupita kufanya kazi hiyo mkoa hado mkoa pamoja na kuwashukuru baada ya kuwachaguwa wabunge wa chadema”alisema Mbowe .