Adverts

Feb 24, 2011

CHADEMA YAANGUSHA GHARIKA MWANZA SAUTI ZA WANYONGE ZARINDIMA...UUUuuuu!! MAANDAMANO YAMALIZIKA KWA AMANI TELE.

"Freeman Mbowe, Dk. Willibrod Slaa pamoja na mawaziri wake vivuli, leo wameliteka Jiji la Mwanza na viunga vyake kwa kupata mapokezi makubwa.@ MBOWE-'Tutawaunganisha watu wote wawe kitu kimoja tudai ukombozi wa pili wa kweli ulio halali kwa nchi hii' Dr. SLAA Maandamano yalianzia Kata ya Nyakato, Buzuruga na kupita barabara za Nyerere, Pamba, Kenyatta, Makongoro na hatimaye kuhitimishwa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kwa mkutano. Mh. Sugu pale kati pembeni mwa diwani wa Mwaloni 'MBISHI'(sifa) Novat Manoko. Takribani wabunge 48 wanao wakilisha Chadema toka mikoa na wilaya mbalimbali hapa nchini wamehudhuria maandamano hayo na mkutano wake Mwanza. Mbowe ambaye alionekana akizungumza kwa umakini mkubwa na kwa msisitizo, amesema yeye na timu yake wamekuja Mwanza kuwasha moto wa maandamano makubwa ya amani kwa muda wa siku tatu, leo katika wilaya za Nyamagana na Ilemela, kisha kuanzia kesho Ukerewe, Misungwi, Geita na Sengerema. Sanaa nayo haikuachwa nyuma kuhusishwa katika kunakshi sherehe. CHADEMA wamesema kuwa Moto kama huu wataendelea kuuwasha katika mikoa ya Mara, Shinyanga, Mkoa mpya wa Simiyu na hatimaye Mkoa wa Kagera. Mwisho wa siku wananchi haoooo...warejea makwao kwa amani na utulivu hakuna aliyeumia wala kupigwa kwenzi licha ya umati kufurika katika maandaamano na uwanjani Furahisha.
"