Adverts

Feb 24, 2011

MAANDAMANO YA CHADEMA YANAYOENDELEA SASA JIJINI MWANZA NI NOMA..

Chama cha maendeleo na demokrasia nchini CHADEMA leo kimefanya maandamano ya amani katika jiji la Mwanza kupinga kupinga mchakato wa uchaguzi na matokeo ya Meya wa Jiji la Arusha, kuunga mkono maandamano yaliyofanywa na chama hicho mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu na kupinga zoezi la serikali kulipa deni la Dowans.Maelfu ya wakazi wa jiji la Miamba muda huu wamejitokeza kwa wingi kuliunga mkono zoezi hili ambalo limeanzia eneo la Buzuruga wilaya ya nyamagana na kuelekea katika viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela ambapo kutakuwa na mkutano. MabangozZZZ!!.. Hali ya hewa barabara ya Kenyeta. Mmiliki wa dowans aka..... Barabara ya Makongoro kuelekea kata ya Kirumba uwanja wa Furahisha eneo ambako mkutano utafanyika jioni ya leo. Ujumbe kwa wakazi wa Gongo la mboto toka CHADEMA Mwanza. Pikipiki eneo la kipita shoto cha ilipokuwa sanamu ya baba wa taifa.
"