Adverts

Feb 24, 2011

CHRIS BROWN 'RUKSA' KUMSOGELEA RIHANNA!

Kwa sasa hatimaye kile kizuizi alichokuwa amewekewa artist Chris Brown kumkaribia mpenzi wake wa zamani Robyn Rihanna Fenty aka Rihanna kimetenguliwa rasmi jijini Los Angeles-Marekani.

Wanasheria wa Rihanna walikubali kupunguzwa kwa masharti hayo na kwa sasa Chris Brown ruksa kuwa karibu na Rihanna sababu imetimia karibu miaka 2 tangu Chris Brown alipompiga Rihanna kwenye tuzo za Grammy za mwaka 2009,na kupewa adhabu ya kazi za jamii na vilevile kutokua karibu na mtoto Rihanna hata kwenye show,party au mualiko wowote kama angekwenda angekua amevunja sheria.

"