Adverts

Feb 24, 2011

Gadaffi anywea mwanae abwabwaja waandamanaji wazidi kupeta

Mtoto wa imla wa Libya, Al Islam Gadaffi kachafua hali ya hewa kwa kuongeza mafuta kwenye moto. Amelaumu jeshi kwa kutokuwa na viwango huku akikanusha mauaji ya wazi ya watu zaidi ya 172. Kijana ambaya hana mamlaka yoyote kisheria amebwabwaja hadi kuahidi kubadili bendera na wimbo wa taifa kama waandamanaji watapenda. Kwa waliomtazama kwenye runinga wametoka na picha moja-Gadaffi kwisha kazi yake. Na inavyoonekana, haitachukua muda mrefu kama Misri au Tunisia. Wengi tumeshangaa mantiki ya kulaumu jeshi wakati bila jeshi hawa wezi hawana pa kushika. Mji wa Benghazi umeishakamatwa na waadamanaji na habari zaidi zinasema waandamanaji wanaelekea Tripoli kutoka miji ya jirani. Benghazi ni sherehe za kuanguka utawala dhalimu wa miaka 42 ya imla Gadaffi. Mtoto wa Gadaffi akiwa amechanganyikiwa wazi, ametoa mpya kwa kusema eti waandamanaji wamefanya hivyo kutokana na kutumia mihadarati! Ni vituko vitupu. Tuzidi kuomba wimbi hili liendelee na kushuhudia kihiyo huyu akiondolewa kwa aibu zote. Wengi walizoea kumuona Gadaffi kama mtu jasiri. Kumbe, kama Saddam Hussein, ni hovyo tu! Kuna uvumi kuwa Gadaffi mwenyewe ameishakimbia nchi.
"