Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa (kulia) akimpatia taarifa Waziri wa Ujenzi Mhe. Dr. John Magufuli (Mb) kuhusu maendeleo ya miradi mbali mbali inayotekelezwa chini ya ufadhili wanchi ya Japan.
Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa amemtaarifu Waziri wa Ujenzi Mhe. Dr. John Magufuli (Mb) kwamba, Serikali ya Japan itahakikisha kuwa ujenzi wa sehemu ya barabara kati ya eneo la Mwenge na Tegeta katika barabara inayounganisha mji wa Dar es Salaam na Bagamoyo, inaanza kujengwa mapema ifikapo mwezi Aprili mwaka huu na kukamilika katika ndani ya muda na kwa viwango vilivyoanishwa katika mkataba.
Kampuni ya Ujenzi ya Konoike kutoka Japan mnamo mwezi Desemba mwaka jana iliingia mkataba wa upanuzi wa barabara kuanzia sehemu ya Mwenge hadi Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9. Ujenzi huo unagharimu kiasi cha fedha za Kijapani Yen 4.55milioni ujenzi wake unakadiriwa kuchukua miezi 29.