Rais wa TFF, Leodegar Tenga akipongezwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Uganda (FUFA) Lawrence Mulindwa mara baada ya kuchaguliwa Februari 23 mwaka huu kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Afrika (CAF) katika uchaguzi uliofanyika jijini Khartoum, Sudan.
(Picha na Fredrick Kiyingi wa Uganda's Daily Monitor)
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) wakimpongeza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga baada ya kuchaguliwa Februari 23 mwaka huu jijini Khartoum, Sudan kuingia kwenye Kamati ya Utendaji.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani (kushoto) na Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye wakimpongeza Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya kuchaguliwa Februari 23 mwaka huu jijini Khartoum, Sudan kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).