Adverts

Feb 7, 2011

MAONI YA PROFESA MBELE KATIKA MADA YA KAZI YA UALIMU: TAALUMA MUHIMU ILIYODHARAULIWA

MAONI YA PROFESA MBELE KATIKA MADA YA KAZI YA UALIMU: TAALUMA MUHIMU ILIYODHARAULIWA: "Maoni haya yalitolewa na profesa Mbele tareha 3/2-2011 kwanye mada hii hapa.
Hapa ni mwenyewe profesa J.Mbele
Na hivi ndivyo alivyosema;-
Mimi ni mwalimu, na nilikuwa na wito wa kuwa mwalimu tangu nilipokuwa mdogo, sijaanza hata shule. Kila siku najitambua kuwa niliitwa na Muumba kuwa mwalimu, na sijawahi kutetereka hata siku moja, pamoja na magumu yake. Nitatoa mifano miwili ya magumu hayo. Nilianza ualimu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1976, baada ya kuhitimu shahada ya kwanza. Baina ya mwaka 1980-86 nilikuja Marekani kusomea shahada ya uzamifu. Nilifanya juhudi masomoni, hadi kupata tuzo ya mwanafunzi bora, nikanunua vitabu vingi sana, kwa kuelewa kuwa ndio nyenzo nitakayohitaji wakati wa kurejea tena Chuo Kikuu Dar kuendelea kufundisha. Nilirejea nchini ule mwaka 1986 na shehena kubwa ya vitabu. Wa-Tanzania waliniuliza kama nimeleta gari ('pick-up'). Kwa vile sikuwa nimeleta gari, bali hivyo vitabu, waliniona nimechemsha. Hii ndio hali halisi, ambayo kwangu ni ngumu. Kwa mtazamo wangu, mwalimu si mtu anayefundisha darasani tu, bali anatakiwa kuwa mfano kimaisha. Nami nilijaribu kuonyesha mfano wa kuthamini elimu. Kinachonitatiza akilini ni kujiona ninajaribu kuwafundisha watu ambao akili zao ziko kwenye magari, na hapo darasani wanatafuta vyeti tu waende zao kusaka mali. Si kwamba wanathamini elimu kama elimu. Hawanioni mimi mwalimu kama mtu ninayewapa mfano wa kutambua nini kitu muhimu maishani, yaani elimu. Suala la kuwasukuma wa-Tanzania watambue umuhimu wa elimu lina usumbufu na kero nyingi, kama alivyoelezea Profesa Matondo hapa.
"