Adverts

Feb 9, 2011

Mmiliki wa TV kufungwa maisha kwa kumuua mkewe?

Mmiliki wa TV kufungwa maisha kwa kumuua mkewe?: "
Aasiya and Muzzammil Hassan

marehemu Aasiya na bwana Muzzammil Hassan enzi za ndoa yao

Mfanyibiashara wa kimarekani mwenye asili ya Mashariki ya Kati, Muzzammil Hassan, amepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji ya aliyekuwa mkewe bi. Aasiya. Mwanamama huyo alipoteza maisha wiki moja baada ya kutalikiana na mwanaume huyo wa Kipalestina, ambapo ilionekana kuwa mwanaume huyo alihusika katika kifo chake.

Na baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wapelelezi nchini Marekani, mmiliki huyo wa kituo cha Televisheni chenye kurusha hewani vipindi vya dini ya kiislamu, amekutwa na hatia ya kuhusika na mauaji hayo, hali ambayo huenda ikampeleka jela maisha endapo atashindwa kuzithibitishia mahakama pasi na shaka kuwa hakuhusika.

Soma zaidi kwa kubonyeza hapa.

"