Adverts

Feb 9, 2011

msondo kutoa burudani tamasha la michezo la wanahabari, airtel kumwaga zawadi kibao kwa washindi

msondo kutoa burudani tamasha la michezo la wanahabari, airtel kumwaga zawadi kibao kwa washindi: "
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Muganyizi Mutta (kulia) akionyesha moja ya kombe litakalotolewa kama zawadi katika tamsha la wanahabari la ‘Airtel All Media Bonanza ‘ litakalofanyika Jumamosi wiki hii katika viwanja vya TTCL Kijitonyama, Dar es Salaam.Kushoto ni Mratibu wa tamsha hilo Mawazo Waziri wa Capital Plus international (CPI). Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Muganyizi Mutta (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya tamsha la wanahabari la ‘Airtel All Media Bonanza ‘ litakalofanyika Jumamosi wiki hii katika viwanja vya TTCL Kijitonyama, Dar es Salaam.Kushoto ni kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma itakayotumbuiza siku hiyo Said Mabela.
Rapa na mwimbaji wa bendi ya Msondo Ngoma Roman Mgande ‘Romarii’ (kushoto) akionyesha manjonjo yake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) walipotambulishwa kama bendi itakayotoa burudani katika tamsha la wanahabari la ‘Airtel All Media Bonanza ‘ litakalofanyika Jumamosi wiki hii katika viwanja vya TTCL Kijitonyama, Dar es Salaam.Kulia ni kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma itakayotumbuiza siku hiyo Said Mabela.
Airtel Tanzania leo imetangaza zawadi za washindi wa michezo tofauti zitakazotolewa katika tamasha la wanahabari litakalofanyika Jumamosi wiki hii katika viwanja vya TTCL Kijitonyama, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Meneja Uhusiano wa Airtel Muganyizi Mutta, alisema wameandaa zawadi za kuvutia katika kuongeza hamsa ya ushindani miongoni mwa vyombo vya habari vitakavyoshiriki michezo husika.
Pamoja na vikombe kwa washindi wa mpira wa miguu, pete, kuvuta kamba,kucheza dansi na kuimba lakini pia kutakuwa na zawadi za papo kwa papo kwa michezo mbalimbali ya kubahatisha itakayochezeshwa na kampuni hiyo ambapo pia kutakuwa na zawadi ya kombe kwa ajili ya mshindi wa jumla.
“Tumeandaa zawadi mbalimbali za kuvutia katika kuongeza hamasa na ushindani kwa washiriki lakini pamoja na hilo kutakuwa na zawadi za promosheni kwa michezo tofauti ya kubahatisha itakayochezeshwa na Airtel, yote hayo ni katika kuhakikisha kuwa watakaoshiriki wanaburudika kwa kiwango chake,” alisema Mutta.
Hii ni mara ya pili kwa kampuni ya Airtel iliyobadilishwa jina kutoka Zain kufanya tamasha kwa wanahabari ambapo tamasha la kwanza kama hili kwa wanahabari lilifanyika mwaka 2009.
Kwa upande wa burudani alisema bendi ya Msondo Ngoma “Baba ya Muziki” italipamba tamasha hilo na tayari bendi hiyo ipo kamili kuporomosha burudani katika siku hiyo ya aina yake kwa wanahabari nchini.
Kwa upande wake Mratibu wa tamasha hilo Mawazo Waziri wa kampuni ya Capital Plus International alisema maandalizi yamekamilika na kila kitu kipo katika mstari kusubiri siku ya tamasha ambapo alitoa rai kwa washiriki kuwahi ili ratiba ya michezo iweze kwenda kama ilivyopangwa.
“Wanahabari wamekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii na hivyo Airtel imeona ni kitendo cha uungwana kuandaaa tukio hili maalum kwa wanahabari ambalo litawakutanisha na kuwaburudisha kupitia michezo”. alisema.
Kiongozi wa bendi hiyo Kibiriti aliwaahidi wanahabari burudani ya kipekee siku hiyo na kwamba wamedhamiria kudhihirisha kuwa wao ni ‘baba ya muziki’ wa kweli katika ulimwengu wa muziki wa dansi nchini.
“Tumefurahi kupata mwaliko wa kuwaburudisha wanahabari siku hiyo na sisi hatutafanya makosa tutatoa burudani ya kipekee na kudhihirisha kuwa hakuna mwingine kama msondo katika muziki wa dansi nchini,” alisema Kibiriti.
"