Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi wakifuatilia kwa makini maelekezo katika mafunzo elekezi ya utawala bora yanayoendelea katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo lengo ni kutekeleza yale yaliyomo katika mpango wa maboresho ya serikali za mitaa na hasa uendeshaji wa vikao, majukumu yao na mipaka ya nafasi zao
Mh sinkala akiwa na furaha baada ya kuingia mjengo wa halmashauri kwa ushindi mzito licha ya ulemavu wake, hii ni dalili kuwa wananchi wamekuwa waelewa sasa na kuachana na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu, hongera wapiga kura wa Msangano, ni mfano wa kuigwa.
Diwani wa Tunduma kupitia CHADEMA akiandika point aliyoinasa katika uwasilishaji wa mwezeshaji wa mafunzo hayo